Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance
Israel imesema imepokea miili ya mateka watatu kutoka kwa wanamgambo wa Hamas.
Hii ni kama sehemu ya mpango wa kubadilishana wafungwana mateka ulioko chini ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Marekani.
Msemaji wa wizara ya afya ya Israel amesema kuwa miilihiyo imewasili katika kituo cha kitaifa cha uchunguzi kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi wa mazingira na sababu za vifo.
Wanamgambo wa Hamas wamesema wameipata miili hiyo katika njia mojawapo ya kuelekea kwenye mahandaki ya kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Wanamgambo hao walikuwa wakiwashikilia mateka 48 huko Gaza wakiwemo 20 ambao walithibitishwa kuwa hai wakati makubaliano ya kusitisha mapigano yalipotangazwa.
Tangu kuanza utekelezwaji wa makubaliano hayo, Hamas imewaachia mateka wote waliokuwa hai na ikaanza mchakato wa kuiwasilisha miili ya mateka 28 waliofariki dunia.
Israel inaituhumu Hamas kwa kujikokota katika zoezi hilo la kuirejesha miili hiyo ila wanamgambo hao wanalalamikia ugumu wa kuifukua miili hiyo iliyofunikwa na vifusi vya majengo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.