Afghanistan yakumbwa na tetemeko kubwa la ardhi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Uharibifu uliotokana na tetemeko la ardhiPicha: AFP

Tetemeko la ardhi lenye uzani wa 6.3 kwenye vipimo vya richter limeipiga Afghanistan usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu 7 na kuwajeruhi wengine 150.

Idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka. Tetemeko hilo limepiga karibu na mojawapo ya miji mikubwa ya Afghanistan wa Mazar-e Sharif.

Kulingana na shirika la kuchunguza matetemeko ya ardhi la Marekani la USGS, lilipata tahadhari katika mfumo wake, inayoonyesha kuwa kuna uwezekano wa wahanga wengi kutokana na tetemeko hilo na kwamba kuna uwezekano wa kuwa janga hilo limefanyika katika maeneo mengine pia.

Tetemeko hilo limepiga kina cha kilomita 28 ardhini na karibu na Mazar-e Sharif, mji ulio na karibu watu 523,000.

Shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga huko Afghanistan limesema litatoa taarifa kuhusiana na vifo au hasara zitatolewa baadae.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ukubwa wa hasara ya tetemeko hilo kwa wakati lilipotokea.

Video za juhudi za kuwaokoa watu waliokuwa wamenasa chini ya vifusi zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii. 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment