Polisi Tanzania: Tunachunguza uwepo wa wahalifu wa nje

Polisi TanzaniaPicha: Ericky Boniphace/DW

Taarifa hiyo ya polisi iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii inasema watu hao wapo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Songwe na Arusha.

Jeshi la polisi nchini Tanzania limesema leo Jumapili kwamba limepata taarifa za kuwepo nchini humo kwa watu wasiokuwa raia wa Tanzania , walioingia kwa njia zisizo rasmi kwa nia ovu ya kufanya uhalifu na vurugu.

Taarifa hiyo ya polisi iliyochapishwa katika  mitandao ya kijamii inasema watu hao wapo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Songwe na Arusha.

Taarifa hiyo inakuja siku chache baada ya vurugu, machafuko na maandamano ya umma ya kupinga uchaguzi mkuu katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Uharibifu mkubwa na vifo vingi vinatajwa kutokea hasa katika mikoa hiyo iliyotajwa katika taarifa hiyo ya polisi. Kwa mujibu wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA ni kwamba mamia ya watu wameuwawa huku ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikisema ina taarifa za kuaminika zinazoonesha watu kiasi 10 wameuwawa katika miji mitatu nchini humo. 
 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment