Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV.Picha: Filippo Monteforte/AFP
Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani, ametowa mwito wa kuanzishwa mazungumzo badala ya machafuko.
Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV , ameizungumzia hali inayoendelea nchini Tanzania hivi leo Jumapili kwa kutowa mwito kwa pande zote kujiepusha na machafuko na badala yake kufuata njia ya mazungumzo.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki imetumbukia katika hali mbaya ya vurugu za kisiasa zilizosababishwa na uchaguzi uliopingwa na umma wa Watanzania.

Vurugu za maandamano ya kupinga uchaguziPicha: AP Photo/picture alliance
Chama kikuu cha upinzani CHADEMA kinaamini mamia ya watu wameuwawa huku ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikisema ina taarifa za kuaminika zinazoonesha watu kiasi 10 wameuwawa katika miji mitatu nchini humo.
Papa Leo ameizungumzia pia hali ya Sudan
Ama kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki duniani Papa Leo ametowa mwito pia wa kusitishwa mara moja kwa vita nchini Sudan na kufunguliwa kwa njia za kupitisha msaada wa kiutu.
Papa Leo amesema, amekuwa akifuatilia kwa masikito makubwa ripoti zinazoonesha ukatili wa hali ya juu unaofanyika katika mji wa Al Fashir katika jimbo la Darfur.
Katika hotuba yake kwa waumini ya kila wiki kwenye sala ya Jumapili katika uwanja wa kanisa la mtakatifu Petro, huko Vatican Papa Leo ametaja juu ya mashambulizi ya kiholela dhidi ya wanawake na watoto na raia wasiokuwa na hatia kwa ujumla wake akisema ni hujuma inayozuia hatua ya kutowa msaada na kusababisha mateso yasiyokubalika.

Kikosi cha wanamgambo wa RSF wakidhibiti mji wa El-Fasher – DarfurPicha: Rapid Support Forces/AFP
Kadhalika ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukuwa hatua thabiti kusaidia juhudi za kutowa msaada.
Ofisi ya haki za binadamu ya UN siku ya Ijumaa ilisema mamia ya raia na wapiganaji wasiokuwa na silaha huenda wameuwawa mwishoni mwa mwezi Oktoba baada ya wanamgambo wa RSF kuuteka mji wa Al Fashir uliokuwa ngome ya mwisho ya wanajeshi wa serikali katika jimbo la Darfur.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.