ZEC: Dkt. Hussein Ali Mwinyi ndiye mshindi wa urais Zanzibar

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mwinyi cheti chake cha urais, baada ya kumtangaza kuwa shindi wa uchaguzi wa rais ZanzibarPicha: Zanzibar Electoral Commission

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC imemtangaza Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa kujizolea zaidi ya asilimia 74 ya kura, katika zoezi la uchaguzi wa Oktoba 29.

Unachohitaji kujua

  • Dkt. Hussein Ali Mwinyi atangazwa mshindi wa urais Zanzibar 
  • Matokeo yaendelea kutolewa Tanzania, Samia aongoza
  • Wabunge wa Ulaya wasema uchaguzi Tanzania haukuwa wa huru na haki 
  • Waandamanaji wajadili mbinu za maandamano zaidi Tanzania
  • Watanzania waamriwa kubakia nyumbani kufuatia ghasia zinaziendelea

ZEC yamtangaza Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jaji George Joseph Kazi, amemtangaza Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, uliofanyika visiwani humo tarehe 28 na 29 Oktoba 2025.

Jaji Joseph Kazi amesema Rais Mwinyi, aliyefanikiwa kutetea kiti chake kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 74.8 ya kura, akimng’oa mpinzani wake wa karibu Othman Masoud Othman wa ACT-Wazalendo, aliyepata asilimia 23.2 ya kura.

Ushindi huo unampa fursa Dkt. Mwinyi kuendelea na muhula wake wa pili kama Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mwinyi aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2020, ataiongoza Zanzibar kwa miaka mingine mitano hadi mwaka 2030.

Mawakala wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, wakihesabu kura kabla ya matokeo rasmi kutangazwa na Mwenyekiti wa ZEC Jaji Joseph KaziPicha: Zanzibar Electoral Commission

Wapigakura visiwani Zanzibar ndiyo waliokuwa wa kwanza kumiminika vituoni Oktoba 28 kwa kile kilichoitwa “kura ya mapema” ikiwa ni siku moja kabla ya kuungana na wenzao wa Tanzania Bara Oktoba 29, kwenye uchaguzi mkuu 2025.

Kisheria, kura hiyo ya mapema ilihusisha makundi maalumu, wakiwamo maafisa wa ulinzi na usalama na wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), waliokuwa kazini siku ya Uchaguzi Mkuu. Makundi hayo yalipewa fursa hiyo ya kupiga kura mapema ili kuhakikisha ushiriki wao unalindwa bila kuathiri majukumu yao ya kitaifa.
 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment