Mkuu wa jeshi Tanzania alaani vurugu zinazoendelea

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuwa jeshi linashirikiana na vyombo vingine vya usalama kudhibiti hali ya usalama nchini humo.

Mkuu wa jeshi nchini Tanzania amelaani vitendo vya vurgu vinavyoendelea kote nchini humo na kuvitaja kuwa kinyume cha sheria.

Katika hotuba yake iliyorushwa na televisheni ya taifa, Jenerali Jacob John Mkunda alisema ni lazima utawala wa sheria uzingatiwe‘ na kuonya kuwa wahusika watachukuliwa hatua.

Aliongeza kuwa jeshi linashirikiana na vyombo vingine vya usalama kudhibiti hali ya usalama huku akiwataka wanaoendesha vurugu hizo kuyakomesha mara moja.

Taarifa hiyo imetolewa wakati maandamano yakizidi kuongezeka katika miji mikubwa.

Mkunda alisema jeshi na vyombo vingine vya usalama vilikuwa vinashirikiana kudhibiti hali hiyo.

Mvutano uliongezeka baada ya matokeo ya uchaguzi kuonyesha Rais Samia Suluhu anaongoza katika maeneo kadhaa.

Waandamanaji wanashutumu serikali kwa kunyamazisha upinzani huku waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakisema uchaguzi ‘haukuwa huru na wa haki’.

Biashara za baadhi ya wasanii wenye kuunga mkono CCM zavamiwa

Vurugu ambazo zimeshuhudiwa nchini Tanzania zimeonekana kulenga watu mashuhuri kama vile wasanii na wanamitindo wanaodaiwa kuunga mkono serikali ba kusababisha kuvamiwa na kuharibiwa kwa biashara zao.

Kufuatia hatua hiyo, baadhi yao wamefuta picha na video walizochapisha kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram zakumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wakiongozwa na msanii wa nyimbo za bongo Naseeb Abdul almarufu Diamond Platnumz wamefuta maudhui hayo waliokuwa wakiyachapisha wakati wa kampuni za uchaguzi mkuu.

Miongoni mwa waathirika wa kwanza ni mwimbaji Shilole, ambaye mgahawa wake maarufu wa Shishi Foods, ulichomwa moto katika machafuko hayo.

Mkuu wa jeshi nchini Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda alitoa taarifa akilaani vurugu zinazoendelea na kusema kuwa ni ‘lazima utawala wa sheria uzingatiwe’ na kuonya kuwa wahusika watachukuliwa hatua.

Ufunguzi wa Vyuo Vikuu Tanzania waahirishwa

Wazara ya Elimu Sayansi naTeknolojia nchini Tanzania imetangaza kuahirishwa kwa ufungui wa vyuo vikuu,vyuo vya elimu ya juu na kati hadi itakapotangazwa tena.

Vyuo hivyo viliatarajiwa kufunguliwa tarehe 3 mwezi Novemba.

Tangazo hilo pia linawajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo ambao walipaswa kujiunga tarehe moja Novemba.

Hussein Mwinyi ashinda uchaguzi wa urais Zanzibar

Mwinyi

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemtangaza Dk Hussein Ali Mwinyi kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais katika visiwa hivyo.

Dk.Mwinyi aligombea kwa tiketi ya chama tawala cha CCM, ambacho hakijawahi kushindwa uchaguzi tangu uhuru.

Zanzibar, eneo linalojitawala ndani ya Tanzania, lilipiga kura siku ya Jumatano.

Mwinyi, aliye na umri wa miaka 59, ameingia kwenye uchaguzi huu wa 2025 akibeba bendera ya CCM kwa mara ya pili mfululizo.

Tangu kuingia madarakani, ameelekeza juhudi zake katika maeneo matatu makuu: utalii, uwekezaji na huduma za kijamii.

Pia amesifiwa kwa kuendesha Zanzibar yenye hali ya utulivu na mshikamano zaidi kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa, tofauti na misuguano ya kisiasa iliyoshuhudiwa kabla ya hapo.

Vurugu za uchaguzi Tanzania: Hali ikoje Mwanza?

Hali ya sintofahamu iliendelea kushuhudiwa mjini Mwanza usiku wa kuamkia leo kutokana na hali ngumu iliyotokana na maandamano ya vijana maarufu Gen Z wakipita katika maeneo mbali mbali ya mji na kuzua hali ya taharuki hasa walipokuwa wakipambana na vikosi vya usalama.

mali Milio ya risasi na mabomu ya machozi ilisikika katika maeneo kadha wa kadha ya jiji hilo.

Kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi kuelekea eneo la Buhongwa waandamanaji wameripotiwa kufukuzana na polisi baada ya kituo cha polisi kuteketezwa.

Katika barabara kuu kutoka Mwanza mjini kuelekea eneo la uwanja wa ndege waandamanaji walipambana na polisi wamekuwa wakipambana vilivyo na ofisi ya kata na kituo kidogo cha polisi nacho kikachomwa moto. Katika eneo la Nyamanolo mkabala na Fwatiati hali sio shwari kwani huko pia kituo cha polisi na ofisi ya kata ya CCM kilichomwa moto.

Waandamanaji pia walivamia duka kubwa la jumla yaani Super Market na kulipora.

Raia wa Uingereza walioko Tanzania watakiwa kuchukua tahadhari

.

Raia wa Uingereza wanaoishi nchini Tanzania wameshauriwa kuchukua tahadhari na kujilinda kufuatia ghasia na maandamano yanayoendelea kuripotiwa nchini humo.

Kulingana na taarifa ya ubalozi wa Uingereza iliotolewa tarehe 30 Oktoba, ubalozi huo aidha umewashauri raia wake wafuate amri zinazotolewa na serikali ya Tanzania kipindi hiki.

‘Zingatieni amri ya kutotoka nje, fuata ushauri wa serikali za mitaa na pia epukeni maandamano’, yasema taarifa hiyo.

Serikali yaonya Wakenya dhidi ya kushiriki maandamano ya Tanzania

.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Raymond Omollo amewaonya Wakenya dhidi ya kushiriki maandamano kinyume cha sheria mpakani mwa Kenya na Tanzania, akionya kuwa yeyote atakayepatikana akisababisha fujo atakabiliwa na sheria.

Onyo lake linafuatia ripoti za maandamano katika vituo kadhaa vya mpakani, ikiwa ni pamoja na Namanga, ambapo baadhi ya wakazi waliripotiwa kuingia barabarani kwa mshikamano na Watanzania kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatano.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Mombasa, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Kenya ina sheria na kanuni wazi zinazosimamia maandamano na kuwataka raia kuendesha shughuli zao ndani ya mipaka ya kisheria.

“Kama nchi, tuna sheria na kanuni zinazoongoza maandamano. Wito wangu ni kwamba yeyote anayetaka kushiriki katika shughuli kama hizo lazima afanye hivyo kwa mujibu wa sheria,” alisema Omollo.

Hakutaka kuzungumzia hali nchini Tanzania, akibainisha kuwa ni suala la ndani kwa nchi hiyo jirani.

“Nisingependa kuzungumza na kile kinachotokea Tanzania. Ni majirani zetu marafiki na tunawatakia kila la kheri wanapopitia michakato yao ya kidemokrasia,” alisema. Waziri pia aliwahimiza wakazi na wafanyabiashara wanaofanya kazi kando ya mpaka kushirikiana na mamlaka ili kuepuka usumbufu wakati wanaendesha shughuli zao.

“Ikiwa kuna usumbufu wowote…, maafisa katika vituo vyetu vya kuingia na kutoka mpakani watatoa mwongozo ili kuhakikisha usalama wa maisha na mwendelezo wa biashara”, aliongeza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment