WEKEZA NGUVU KUBWA KATIKA MAENEO HAYA 3 ILI KUKUZA BIASHARA YAKO.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Kama unataka biashara yako ikue na mauzo yaongezeke, kuna jambo moja muhimu unalopaswa kuelewa kuwa wateja ndio moyo wa biashara. Bila wateja, hakuna biashara.

Lakini je, unajua kuwa kuna hatua tatu muhimu unazopaswa kupitia ili kuvutia na kudumisha wateja? Hizi Hapa …

1. KUTAFUTA WATEJA.

Hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa. Kabla mtu hajawa mteja wako, lazima ajue kuwa biashara yako ipo.

Jitangaze vya kutosha usikae kimya ukitarajia watu wakufuate. Tumia mbinu zote za kutangaza,mitandao ya kijamii kama instagram, Facebook, TikTok unaweza kuwezesha kwa kutumia matangazo ya kulipia (Sponsored Ads) na Bajaji, mabango, vipeperushi na Redio za kijamii au za mikoa

Ongea na watu, shiriki maonesho ya biashara, tumia referrals, Wateja wa mwanzo ndio watakaokuletea wengine. Waambie watu kuhusu huduma au bidhaa zako.
Ni jukumu kama mfanyabiashara kuweka mikakati ya kutafuta wateja wapya.

2. KUWAHUDUMIA WATEJA.

Baada ya kuwavuta wateja, sasa ni wakati wa kuhakikisha wanafurahia huduma yako.

Unapaswa kuwahudumia kwa viwango vya juu,kwa kuwapa bidhaa au huduma bora, bila udanganyifu,kuwa na mapokezi mazuri Kwa mfano karibu mteja kwa heshima na tabasamu.

Na Wape suluhisho la changamoto zao sio tu kuuza, bali kuweza kuwasaidia. Lakini pia wape maudhui (content) tofauti mara kwa mara za kuelimisha, kuhusu bidhaa zako,na pia kuhusu shuhuda.

Katika kuwahudumia wateja unahitaji kujibu maswali yao kwa haraka na kwa heshima
Lakini pia wape neno la kuwashukuru wanapoondokaBila huduma nzuri kwa wateja hauwezi kupata matokeo makubwa.

3. KUWATUNZA WATEJA

Wateja waliokwisha nunua kwako ni dhahabu usiwaache waondoke kirahisi. Watunze ili wabaki kwako milele.

Unahitaji kuwasiliana nao mara kwa mara, save namba zao kwa majina yao, mizigo ikiingia wapigie au watumie ujumbe, na tumia WhatsApp Broadcast kuwapa updates

Pata mrejesho wa baada ya kutumia bidhaa zako au huduma zako zimewezaje kuwasaidia.?

Na wape zawadi au OFA maalum, toa zawadi ndogo kwa wateja wa kudumu, au ofa za sikukuu mfano “Discount ya Krismasi”,Kadi za birthday, ujumbe wa heri katika siku zao muhimu.

Mfano mzuri ni kampuni kama Vodacom ambayo hutuma salamu za sikukuu kwa wateja wake na kuwapa ofa za dakika bure kwenye siku za kuzaliwa. Huu ni utunzaji wa mteja fanya vivyo hivyo kwenye biashara yako.Utapata matokeo makubwa.

Ukizingatia haya mambo matatu kikamilifu, utapata wateja wengi, utawafanya warudi tena na tena, na mwisho wa siku, biashara yako itakuwa na mauzo makubwa na mafanikio ya kudumu.

Ni jambo gani bado linakusumbua kuhusu wateja. Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.

Share ujumbe huu kwa wafanyabiashara wengine ili kuweza kupata mafanikio makubwa kwenye biashara zao.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment