Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Wanajeshi wa Lebanon katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na IsraelPicha: Karamallah Daher/REUTERS
Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limefanya uvamizi kusini mwa Lebanon. Duru za habari ziliripoti kuwa vikosi vya Israel vilivamia jengo la manispaa na kumuuwa mwajiriwa Ibrahim Salameh akiwa amelala.
Israel kwa upande wake imebainisha kuwa mashambulizi hayo ya usiku wa kuamkia Alhamisi yalikuwa operesheni dhidi ya miundombinu ya kundi la Hezbollah na Salameh alikuwa mtuhumiwa.
Rais wa Syria aamuru jeshi kukabiliana na uvamizi wowote
Wanakijiji walioshuhudia tukio hilo wamesema uvamizi wa Israel ulidumu kwa saa kadhaa na kuwa wanajeshi waliondoka mapema alfajiri. Kufuatia mashambulizi hayo Rais wa Lebanon Joseph Aoun ameliamuru jeshi kukabiliana na vitendo vya aina hiyo ili kulinda mipaka na wananchi wake.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.