Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri wa mambo ya kigeni Johann Wadephul alipowasili Syria 30.10.2025Picha: Marcus Brandt/dpa/picture alliance
Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amekutana leo na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Johann Wadephul katika juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Ni katika ziara ya kwanza ya Wadephul nchini Syria baada ya ziara mbili za mtangulizi wake Annalena Baerbock ambaye mwezi Machi alifungua ubalozi wa Ujerumani mjini Damascus.
Ushirikiano wa kisiasa, uchumi na masuala ya kiutu kuimarishwa
Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema mazungumzo hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na masuala ya kiutu.
Itakumbukwa kuwa Ujerumani iliwapokea maelfu ya wakimbizi kutoka Syria wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kipindi cha miaka 14. Akiwa na ujumbe wake, Wadephul anatarajiwa kuelekea Lebanon na Bahrain katika ziara yake Mashariki ya Kati.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.