Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Miti ikiwa imeanguka baada ya kupigwa na kimbunga MelissaPicha: Matias Delacroix/AP Photo/dpa/picture alliance
Kimbunga Melissa kinatajwa kuwa ni kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kuwekwa kwa rekodi za vimbunga miaka 174 iliyopita katika maeneo hayo. Asilimia sabini na saba ya kisiwa cha Jamaica bila ya umeme.
Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbungaMelissakilichopiga mataifa ya Karibea imeongezeka. Kimbunga hicho kimewaua watu nane nchini Jamaica na watu wasiopungua ishirini na tano nchini Haiti.
Wakati jitihada za uokozi zikiendelea, Kituo cha Kitaifa cha Marekani kinachoshughulikia vimbunga kimetoa tahadhari kwamba huenda kukawa na ongezeko kubwa zaidi la dhoruba katika maeneo hayo.
Kimbunga Melissa kinatajwa kuwa ni kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kuwekwa kwa rekodi za vimbunga miaka 174 iliyopita katika maeneo hayo.
Inaelezwa kwamba kimbunga hicho kimeiacha asilimia sabini na saba ya kisiwa cha Jamaica bila ya umeme.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.