Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam Jumanne Muliro ametangaza amri ya kutotoka nje jijini humo kuanzia leo saa kumi na mbili jioni.
”Jeshi la polisi kufuatia hali hiyo inawatangazia wakaazi wote wa jiji la Dar es Salaam .kuwa kuanzia leo tarehe 29 Oktoba mwaka 2025 kuanzia saa kumi na mbili jioni wawe majumbani mwao,” alisema Muliro akitoa tangazo hilo.
Hayo ni kufuatia matukio ya ghasia yaliyoshuhudiwa katika maeneo kadhaa mjini Dar Es Salam na kwingineko nchini humo ambapo waandamanaji wanaopinga kufanyika kwa uchaguzi wameandamana wakifunga barabara kadhaa na kuchoma moto maeneo kadhaa.Mshirikishe mwenzako, Amri ya kutotoka nje yatangazwa Dar es Salaam
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.