Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Johann WadephulPicha: Marcus Brandt/dpa/picture alliance
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amezitaka Israel na Hamas kutohatarisha mpango wa amani kwa Gaza, huku mapigano yakipamba moto tena katika eneo hilo licha ya makubaliano ya kusitisha vita.
Kabla ya kuanza ziara ya siku kadhaa Mashariki ya Kati, Wadephul amesema juhudi zote lazima sasa zilenge kukidhi matarajio ya watu katika eneo zima.
Waziri huyo alitoa wito kwa Hamas kutimiza wajibu wake chini ya mpango huo wa amani unaosimamiwa na Marekani, unaolihitaji kundi hilo kusalimisha silaha zake na kurejesha mabaki ya mateka wote wa Israel.
Wadephul aitaka Israel kuepusha mashambulizi zaidi
Pia ameihimiza Israel kutofanya mashambulizi zaidi kuepusha mateso mapya.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya mashambulizi ya Israel Gaza na akazitaka pande zote mbili kuzingatia makubaliano ya amani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.