Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Afisa wa polisi ajaribu kumkamata mfuasi wa upinzani nchini TanzaniaPicha: Emmanuel Herman/REUTERS
Maandamano yenye ghasia yamezuka leo jijini Dar es Salaam, Tanzania wakati wa uchaguzi ambao Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushinda kufuatia kuenguliwa kwa wagombea wakuu wa upinzani.
Mamia ya waandamanaji wamefanya maandamano kuelekea eneo la Daraja la Selander linaloelekea katikati mwa Dar es Salaam. Haya ni kwa mujibu wa shuhuda mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.
Walioshuhudia, wameripoti maandamano ya ghasia katika vitongoji visivyopungua vinne Dar es Salaam, huku video ya shirika la BBC ikionyesha polisi wakitumia gesi za machozi kuwatawanya waandamanaji katika eneo lingine la jiji.
Huduma za mtandao zakatizwa nchini Tanzania
Kundi linalofuatilia huduma za mtandao NetBlocks, limesema huduma hizo zimekatizwa kote nchini humo huku video ambazo hazijathibitishwa za waandamanaji wakiwarushia mawe maafisa wa uslama na pia kuteketeza kituo cha mafuta zikisambazwa mitandaoni.
Msemaji wa serikali na polisi hakujibu mara moja ombi la kutoa tamko kuhusu hali hiyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.