Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Maafisa wa uokoaji kwenye eneo la shambulizi la Urusi nchini UkrainePicha: Vyacheslav Madiyevskyy/REUTERS
Ukraine imeshambulia miundo mbinu ya nishati ya Urusi kwa droni na kutatiza usafiri wa anga kote nchini humo pamoja na kufanya mashambulizi kuelekea mji mkuu wa nchini hiyo Moscow kwa siku ya tatu mfululizo.
Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa Telegram, gavana wa rasi ya Crimea, aliyechaguliwa na Urusi Sergei Aksyonov, amesema chombo kilichokuwa kimehifadhi mafuta mjini Simferopol kilishambuliwa na droni ya Ukraine na kushika moto.
Hata hivyo amesema hakuna vifo vilivyoripotiwa huku huduma za dharura zikifanya kazi katika eneo hilo.
Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Telegram kwamba vikosi vyake ya ulinzi wa anga vilidungua takriban droni 100 za Ukraine usiku kucha ikiwa ni pamoja na sita kwenye eneo la Moscow na nyingine kwenye maeneo 11 ya rasi hiyo ya Crimea.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.