Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Lori la shirika la WFP lasafirisha bidhaa za msaada kutoka mji wa Port Sudan SudanPicha: Abubakar Garelnabei/WFP/Handout/REUTERS
Serikali ya Sudan imemfukuza mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini humo Laurent Bukera, pamoja na mratibu wake wa masuala ya dharura Samantha Chattaraj.
Serikali ya Sudan imesema jana kuwa wawili hao wamepewa muda wa saa 72 kuondoka nchini humo.
Hata hivyo haikutoa sababu za uamuzi huo.
Hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Sudan kuchukua hatua kama hiyo dhidi ya Umoja wa Mataifa.
Sio mara ya kwanza kwa Sudan kuwafukuza wafanyakazi wa UN
Mnamo Juni 2023, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes, alitangazwa kuwa mtu asiyestahili kuwa nchini humo.
Alituhumiwa wa kuchochea vita nchini humo, ambavyo vimedumu sasa kwa zaidi ya miaka miwili.
Siku ya Jumatatu, jeshi la Sudan lilitangaza kujiondoa kutoka El Fashir, mji muhimu katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan, na kuuacha chini ya udhibiti wa kikosi cha wanamgambo cha RSF.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.