Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mwili wa mwathiriwa waondolewa kwenye eneo la shambulizi la Israel katika Ukanda wa GazaPicha: Omar Al-Qattaa/AFP
Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limesema mashambulizi ya anga ya usiku kucha yamewauwa takriban watu 104 katika ukanda wa Gaza.
Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal, ameyataja mashambulizi hayo kuwa ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya amani ijapokuwa Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa hakuna kitu kitakayoyumbisha makubaliano hayo aliyoyasimamia.
Shirika hilo ambalo linafanya kazi kama kikosi cha uokoaji chini ya mamlaka ya Hamas, limesema watoto 22 walikuwa miongoni mwa waliouawa pamoja na wanawake na wazee na kuongeza kuwa takriban watu 200 walijeruhiwa.
Hamas yakanusha kuhusika na shambulizi la Gaza
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi la Israel, mwanajeshi mmoja kwa jina Yona Efraim Feldbaum, mwenye umri wa miaka 37, aliuawa huko Rafah wakati gari lao liliposhambuliwa na kile alichotaja kuwa ”adui”
Hata hivyo Hamas imekanusha kuhusika na tukio hilo na ikasisitiza kujitolea kuzingatia makubaliano hayo ya amani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.