Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Watu kadhaa wamejeruhiwa kwenye maandamano katika baadhi ya miji ya Tanzania huku shughuli ya upigaji kura ukiendelea katika uchaguzi mkuu ambao umekumbwa na mvutano.
Waandamanaji waliwasha moto barabarani, kuharibu mabasi, na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye vituo vya mabasi ya mwendo kasi na miundombinu mingine ya umma.
Tumechoka… Tunataka Tume huru ya uchaguzi ili Watanzania wamchague kiongozi wanayemtaka, mmoja wa waandamanaji aliiambia BBC.
Zaidi ya wapiga kura milioni 37 waliosajiliwa kupiga kura katika uchaguzi wa urais na ubunge.
Vyama 16 vidogo, ambavyo havina umaarufu, vimeruhusiwa kugombea urais dhidi ya Rais Samia, ambaye anawania muhula wa pili.
Mgombea pekee wa upinzani, Luhaga Mpina wa Chama cha ACT-Wazalendo, alienguliwa kutokana na taratibu za kisheria.


Mshirikishe mwenzako, Watu kadhaa wajeruhiwa kwenye makabiliano na polisi

Maandamano yasambaa katika baadhi ya maeneo Dar es Salaam

Maandamano katika jiji la Dar es Salaam yanazidi kusambaa kutoka Kimara na yameingia eneo la Magomeni.
Mapema asubuhi vikundi vya vijana vilianza kujikusanya katika eneo la Kimara Kibo kabla ya kuingia barabarani kuziba barabara kabla ya kukabiliana na Polisi.
Maandamano yameshuhudiwa Kimara, Magomeni, Ubungo, Kinondoni, Shekilango na Tandale.
Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa kwa vituo vya mabasi ya mwendokasi, vituo vya kupigia kura, mabasi, na maeneo ya biashara.

Awali Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alionya kuwa vyombo vya dola viko imara kukabiliana na uvunjifu wa amani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.