Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Polisi jijini Dar es Salaam wametawanya kundi la vijana waliokuwa wakijaribu kuandamana katika eneo la Ubongo na Kimara eneo la Kibo, wakati huu wa uchaguzi mkuu unaoendelea nchini.
Maandamano yasambaa katika baadhi ya maeneo Dar es salaam.
Maandamano katika jiji la Dar es Salaam yanazidi kusambaa kutoka Kimara na yameingia eneo la Magomeni.
Mapema asubuhi vikundi vya vijana vilianza kujikusanya katika eneo la Kimara Kibo kabla ya kuingia barabarani kuziba barabara kabla ya kukabiliana na Polisi.
Maandamano yameshuhudiwa Kimara, Magomeni, Ubungo, Kinondoni, Shekilango na Tandale.
Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa kwa vituo vya mabasi ya mwendokasi, vituo vya kupigia kura, mabasi, na maeneo ya biashara.
Awali Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alionya kuwa vyombo vya dola viko imara kukabiliana na uvunjifu wa amani.
Uchaguzi Tanzania: Serikali yatoa onyo uvunjifu wa amani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Chalamila, amesema vyombo vya dola viko imara na tayari kukabiliana na jaribio lolote la uvunjifu wa amani katika jiji hilo, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuvuruga utulivu.
Kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa za uwepo wa kundi la vijana waliodaiwa kujaribu kuandamana katika eneo la Kibo, Kimara, kabla ya polisi kuwatawanya.
“Hata mkiona kuna propaganda za aina yoyote kwenye mitandao kuhusu eneo lolote la Mkoa wa Dar es Salaam, mjue nguvu itakayotumika kudhibiti jambo hilo ni mara saba zaidi ya nguvu iliyotumika kulipanga,” alisema Chalamila.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura, Chalamila alisisitiza umuhimu wa kulinda utamaduni wa amani ambao Tanzania imeujenga kwa miaka mingi, na kuwataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao pamoja na vyombo vya usalama.
“Utamaduni wa taifa letu ni amani. Tukiiharibu amani hii, kwa lugha nyepesi, tutakuwa tumepoteza msingi wa kuwepo kwetu kama taifa. Nimetembea maeneo mbalimbali kuwaambia vijana wajitokeze kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura, lakini wafanye hivyo kwa amani,” alisema.
Chalamila pia alitoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha jiji hilo linaendelea kuwa kitovu cha utulivu, maendeleo na mshikamano wa kitaifa

- Mgombea mwenza kupitia CCM, Balozi Dkt.Nchimbi apiga kura
Chanzo cha picha,CCMMgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akishiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Rais,Mbunge na Diwani katika mtaa wake, eneo la Kilimani, jijini Dodoma leo tarehe 29, Oktoba 2025.
Chanzo cha picha,CCMMshirikishe mwenzako, Mgombea mwenza kupitia CCM, Balozi Dkt.Nchimbi apiga kura - Mgombea Urais UDP: Nikipata, nikishindwa nitapokea
“Nikishinda kura ya urais nitapokea, nikishindwa nitamuunga mkono na kumpongeza yoyote atakayeshinda,” amesema Mgombea urais kupitia chama cha UDP, Saum Rashid mara baada ya kupiga kura.Akizungumza, mapema leo baada ya kupiga kura jijini Dar es Salaam , Saumu alisema ametimiza wajibu wake wa kikatiba na kwamba kura zitaamua.Alisema kuwa iwapo kura hazitatosha basi atajipanga na uchaguzi mwingine.Hatahivyo, Saumu amedai kuridhishwa na utaratibu uliowekwa wa kupiga kura. “Utaratibu uliowekwa na tume ya uchaguzi unaridhisha.Mimi sasa nasubiri matokeo, nina imani na tume itatenda haki,” alisema mgombea huyo.Katika uchaguzi unaoendelea, wagombea uraisi 17 walijitokeza kugombea nafasi hiyo. Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi, matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya saa 72.
Polisi wakabiliana na ‘waandamanaji’ Dar es Salaam

Polisi jijini Dar es Salaam wametawanya kundi la vijana waliokuwa wakijaribu kuandamana katika eneo la Kimara Kibo, umbali wa kati ya Ubungo na Kimara, wakati huu wa uchaguzi mkuu unaoendelea nchini.
Mashuhuda wamesema kundi hilo la vijana lilianza kujikusanya karibu na Kanisa la Ufufuo na Uzima, ambalo lilifungiwa hivi karibuni. Kanisa hilo la Askofu Josephat Gwajima, ambaye alikuwa mbunge wa chama tawala, CCM, kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka huu. Gwajima amekuwa akijulikana kwa misimamo yake ya kupinga vitendo vya utekaji na ukiukwaji wa haki za binadamu, hatua ambayo iliwahi kumuweka kwenye mvutano na mamlaka za serikali.

Hadi kufikia muda huu, polisi wanaendelea kudhibiti hali ya eneo hilo huku magari ya doria yakionekana katika barabara kuu ya Morogoro Road. Hakuna taarifa rasmi za majeruhi wala idadi kamili ya waliokamatwa.
Maandamano haya ni sehemu ya mwitikio wa mitandaoni wa makundi ya wanaharakati na vijana wakitaka mageuzi zaidi ya kisiasa. Hata hivyo, hadi sasa, maandamano hayo yalikuwa hayajashuhudiwa kwa kiwango kikubwa nchini kote.
Uganda: EC yaanza kuidhinisha waangalizi wa uchaguzi mkuu wa 2026
Tume ya uchaguzi ya Uganda imewaalika waangalizi wa shughuli ya uchaguzi kujisajili katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Tume hiyo imesema kuwa imelenga kuwajumuisha waangalizi kama njia ya kufanya uchaguzi mkuu kuwa wazi na wa haki.
Msemaji wa Tume huru ya uchaguzi ya Uganda Julius Mucunguzi amesema kuwa waangalizi walioomba kusajiliwa tayari wamepokea vibali vyao lakini orodha hiyo haitawekwa wazi kwa vyombo vya habari.
”Shughuli ya kusajili waangalizi wa uchaguzi wa Uganda inaongozwa na kifungu cha 160(1) katika sheria ya uchaguzi ambacho kinaruhusu mashirika ya kiraia,vyama vya kisiasa na taasisi zilizoidhinishwa kufuatilia uchaguzi mkuu,” anasema Mucunguzi.
wakati huo huo, mzigo wa mashine 60,000 za uthibitishaji wa wapiga kura kwa kutumia alama za kibayometria uliwasili nchini Uganda Jumatatu, hatua muhimu katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Uganda utakaofanyika Januari 15, 2026.
Rais Yoweri Museveni atawania muhula mwingine wa uongozi baada ya kuwa madarakani kwa takriban miaka 40.
Kuidhinishwa wa Museveni kuwania urais kwa muhula mwingine kumeibua mjadala katika maeneo mengi nchini humo.
Vyama vinne vya kisiasa tayari vimejiondoa katika kinyang’anyiro cha urais, ikiwa ni pamoja na Democratic Party, chama kongwe zaidi cha kisiasa nchini Uganda na Political Front for Freedom [PFF] kilichoanzishwa na Dk. Kizza Besigye, mkosoaji mkubwa wa Museveni.
Kwa mara ya pili mfululizo nchi hiyo itafanya uchaguzi bila mgombea urais mara nne, Dk. Besigye kuonekana kwenye karatasi ya kura. Alikamatwa mwaka jana akiwa Kenya, bado yuko kizuizini kwa mashtaka ya uhaini. Anakanusha makosa yoyote.
Hata hivyo, wakosoaji wanasema Museveni ametawala Uganda kwa mkono wa chuma tangu achukue madaraka kama kiongozi wa waasi mwaka 1986 na ameshinda kila uchaguzi tangu wakati huo.
Wakati wa uchaguzi uliopita wa 2021, alishinda kwa 58% wakati mpinzani wake wa karibu, Bobi Wine alishika nafasi ya pili kwa 34%. Nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu ujao Januari 12 mwaka ujao.
Trump akutana na kiongozi wa Korea Kusini huku makubaliano ya kibiashara yakisuasua

Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung kama sehemu ya hatua ya mwisho ya ziara yake ya barani Asia.
Mkutano huo unakuja wakati ambapo nchi hizo mbili zinajaribu kufikia makubaliano ya kibiashara – ambayo bado yanaonekana kusuasua licha ya mkutano wa faragha uliochukua takribani saa mbili siku ya Jumatano.
Mpango ulikuwa umetangazwa mwishoni mwa Julai ambapo Korea Kusini ingeepuka ushuru mkubwa zaidi wa dola bilioni 350 ya uwekezaji mpya nchini Marekani.
Lakini mazungumzo kuhusu ya muundo wa uwekezaji huo yamekwama.
Nchi hizo mbili zimekuwa washirika wakuu wa jadi- lakini hali ya wasiwasi iliongezeka baada ya mamia ya Wakorea Kusini kuzuiliwa katika msako dhidi ya wahamiaji nchini Marekani mwezi uliopita.
Habari katika Picha: Kimbunga Melisa nchini Jamaica
Kimbunga Melisa sasa kimeondoka Jamaica na kuelekea Cuba kwa kasi ya maili 120 kwa saa.
Huko Jamaica, Waziri Mkuu Andrew Holness ametangaza Jamaica kuwa “eneo la maafa” na anaonya juu ya “athari mbaya.”
Meya wa Montego Bay ameiambia BBC jambo la kwanza watakalofanya ni “kuangalia kama kila mtu yuko hai”








Mafuriko yauwa watu 9 na wengine 5 hawajulikani walipo Vietnam

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha vifo vya takriban watu tisa na wengine watano kutoweka katikati mwa Vietnam, serikali imesema siku ya Jumatano.
Watu sita kati ya waliofariki ni kutoka mji wa Danang, nyumbani kwa mojawapo ya fukwe maarufu nchini humo, na mji wa kale wa Hoi An, serikali imesema katika taarifa yake.
Mafuriko hayo pia yameharibu zaidi ya nyumba 103,000, nyingi zikiwa katika maeneo ya Hue na Hoi An, shirika la maafa la serikali lilisema katika ripoti tofauti.
Vietnam inakabiliwa na dhoruba mbaya za mara kwa mara za mafuriko ambayo husababisha uharibifu mkubwa wa mali, haswa wakati wa msimu wa dhoruba kuanzia Juni hadi Oktoba.
Mvua kubwa inaendelea kunyesha mji mkuu wa zamani wa kifalme ulioorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia, Hue na mji wa kale wa Hoi An, shirika hilo linasema.
Mvua katika eneo hilo imevuka rekodi ya juu katika kipindi cha saa 24 kilichomalizika Jumatatu, na kuzidi milimita 1,000.
Picha zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari vya serikali zinaonyesha sehemu kubwa ya Hoi An imefunikwa na maji ya mafuriko, huku nyumba kadhaa zikiwa zimezama hadi paa.
Vilevile maporomoko ya ardhi yametokea katika maeneo kadhaa, na kukata barabara na kuangusha gridi za umeme, shirika la maafa limesema, na kuongeza kuwa kampuni ya reli ya serikali bado haijaweza kurejesha huduma kati ya mji mkuu wa Hanoi na kitovu cha biashara cha Ho Chi Minh City kufuatia kusimama siku ya Jumanne.
Mvua kubwa itaendelea katikati mwa Vietnam katika muda wa siku mbili zijazo, huku mvua katika baadhi ya maeneo ikizidi milimita 400 kuanzia mapema Jumatano hadi Alhamisi jioni, kulingana na shirika la serikali la utabiri wa hali ya hewa.
Marekani yabatilisha viza ya Mshindi wa Tuzo ya Nobel kutoka Nigeria

Mwandishi na mshindi wa Tuzo ya Nobel kutoka Nigeria, Wole Soyinka amesema siku ua Jumanne kwamba Marekani imefuta viza yakeiliyotolewa mwaka jana na aliambiwa atume ombi tena kama anataka kutembelea Marekani.
Mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 91 anasema mwaka 2016 aliachana kibali chake cha kukaa Marekani (Green Card) na kukataa kukaa kama njia ya kupinga ushindi wa Rais Donald Trump.
Mshindi huyo wa Tuzo ya Nobel amekuwa na vipindi vya kufundisha mara kwa mara katika vyuo vikuu vya Ivy League vya Marekani tangu katikati ya miaka ya 1990 kufuatia Tuzo yake ya Nobel ya Fasihi mwaka 1986.
Siku ya Jumanne, Soyinka aliwaonyesha waandishi wa habari nakala ya barua kutoka Ubalozi Mdogo wa Marekani mjini Lagos ikimtaka apeleke pasipoti yake kwa ajili ya kufutwa kwa viza hiyo.
Ubalozi wa Marekani nchini Nigeria haukujibu ombi la kutoa maoni.
“Sina viza, nimepigwa marufuku kuingia Marekani na ukitaka kuniona unajua pa kunipata,” alisema akimaanisha watu waliopanga kumualika kwenye hafla za Marekani.
Ubalozi wa Marekani nchini Nigeria ulisema mwezi Julai kwamba Wanigeria wanaotaka kusafiri kwenda Marekani kwa viza zisizo za wahamiaji sasa watapokea vibali vya kuingia mara moja kwa miezi mitatu, na kuondoa viza ya hadi miaka mitano, ambayo ilikuwepo hapo awali ambapo mtu angeweza kusafiri kwenda na kutoka mara kadhaa.Mshirikishe mwenzako, Marekani yabatilisha viza ya Mshindi wa Tuzo ya Nobel kutoka Nigeria
Mwanaume afariki baada ya kiti cha magurudumu kugongana na gari la kipa wa Inter Millan

Mwanaume mmoja amefariki dunia baada ya kiti chake cha magurudumu cha umeme kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na kipa wa Inter Milan, Josep Martinez.
Tukio hilo lilitokea katika jimbo la Como, Italy, huku polisi wakisema kiti cha magurudumu kilionekana kuelekea kwenye njia ya gari hilo.
Mamlaka inaendelea kuchunguza mazingira ya ajali hiyo.
“Gari lililokuwa likiendeshwa na kipa wa Inter, Josep Martinez lilimgonga mtu aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu cha umeme akisafiri kando ya barabara katika jimbo la Como,” polisi wa Italia waliambia Reuters.
“Martinez alisimamisha gari lake ili kumsaidia mtu huyo, ambaye alikufa kabla ya kuwasili kwa gari la wagonjwa.”
Klabu hiyo imekataa kuzungumzia tukio hilo.
Martinez amekuwa kipa chaguo la pili wa Inter tangu ajiunge nayo akitokea klabu ya Serie A ya Genoa mwaka 2024.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27, ambaye pia amewahi kuzichezea Las Palmas na RB Leipzig, amecheza mechi 12 akiwa na Inter.
Mhalifu wa ngono afukuzwa Uingereza na kupelekwa Ethiopia

Mhalifu wa ngono ambaye ni mhamiaji aliyeachiliwa kutoka gerezani kimakosa amefukuzwa kutoka Uingereza, serikali imetangaza.
Hadush Kebatu alifungwa jela baada ya kumnyanyasa kingono msichana mwenye umri wa miaka 14 na mwanamke mmoja huko Essex walipokuwa wakiishi katika hoteli ya kuhifadhi waomba hifadhi, lakini akaachiliwa kimakosa na wafanyakazi wa magereza siku ya Ijumaa.
Alirudishwa rumande kufuatia msako wa siku mbili.
Alitiwa katika ndege na kupelekwa Ethiopia Jumanne usiku na kutua asubuhi iliyofuata, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.
Waziri wa Mambo ya Ndani Shabana Mahmood amesema: “Kosa la wiki iliyopita halipaswi kamwe kutokea – na nina hasira kama umma kwamba lilitokea.”
“Nimefanya kila jambo ili kumfukuza Bw Kebatu na kumtoa nje ya ardhi ya Uingereza. Nina furaha kuthibitisha kwamba mhalifu huyu wa kingono amefukuzwa. Mitaa yetu iko salama,” aliongeza.
Kebatu alifukuzwa nchini bila haki ya kurudi, Ofisi ya Wizara ya Ndani ilisema.
Siku ya Ijumaa, alikusudiwa achukuliwe hadi katika kituo cha kizuizini cha wahamiaji ili afurushwe chini ya mpango wa kuwaondoa mapema wahalifu ambao ni raia wa kigeni.
Badala yake, aliachiliwa katika msingi wa “makosa ya kibinadamu.”
Baada ya Polisi wa Essex walipofahamishwa kuhusu kesi yake, alikuwa tayari amezungumza na wananchi katikati mwa jiji kwa usaidizi na akapanda treni kuelekea London.
Alikamatwa kaskazini mwa London siku ya Jumapili asubuhi baada ya mwananchi kuwasiliana na polisi na kusema walimwona karibu na kituo cha Finsbury Park.
Uchunguzi huru utatafuta kubaini jinsi Kebatu alivyoachiliwa huru na ikiwa wafanyikazi walikuwa na uzoefu wa kutosha, mafunzo na teknolojia.
Wakati huo huo, afisa wa gereza amesimamishwa kazi.
Kebatu aliwasili Uingereza baada ya kuvuka kutoka Ufaransa kwa mashua ndogo tarehe 29 Juni, baada ya kusafiri kupitia Sudan, Libya, Italia na Ufaransa.
Kukamatwa kwake mwezi Julai kulizua wimbi la maandamano nje ya Hoteli ya The Bell mjini Epping, ambayo ilikuwa ikitumiwa kuwapokea watu wanaotafuta hifadhi akiwemo Kebatu.
Mahakama ya Chelmsford ilielezwa kwamba Kebatu alijaribu kumbusu msichana mdogo katikati mwa mji, na akatoa maneno ya ngono kwake.
Siku iliyofuata, alikutana na msichana yuleyule na kujaribu kumbusu kabla ya kumnyanyasa kingono yeye na mwanamke mwingine.
Alikanusha mashtaka dhidi yake lakini alipatikana na makosa matano na kuhukumiwa kifungo cha miezi 12, ikiwa ni pamoja na muda ambao tayari alikuwa gerezani akisubiri kesi yake.
Chini ya Sheria ya Mipaka ya Uingereza ya 2007, amri ya kufukuzwa lazima ifanywe wakati raia wa kigeni anapokea kifungo cha kuwekwa ndani cha angalau miezi 12.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.