Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Mawaziri wa ulinzi wa Pakistan na Afghanistan wakisaini makubaliano ya kusitisha mapigano DohaPicha: Qatar MFA
Pakistan imesema leo kwamba mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu na Afghanistan, yameshindwa kuleta suluhu inayoweza kutekelezeka na kuonya kuwa itachukua hatua za kuwalinda watu wake.
Pakistan imesema leo kwamba mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu na Afghanistan, yameshindwa kuleta suluhu inayoweza kutekelezeka na kuonya kuwa itachukua hatua za kuwalinda watu wake.
Waziri wa habari wa Pakistan Attaullah Tarar aliandika kupitia ukurasa wa mtandao wa X akisema inasikitisha kuona kwamba upande wa Afghanistan haukutoa hakikisho lolote katika utatuzi wa masuala ya msingi, baada ya siku nne za mazungumzo ya Istanbul yaliyosimamiwa na Qatar na Uturuki.
Mazungumzo hayo yalilenga kuleta amani baada ya mapigano makali ya mpaka wa nchi hizo mbili jirani za Asia Kusini. Mapigano hayo yalizuka kufuatia milipuko ya mjini Kabul ambayo Afghanistan inayoongozwa na Taliban iliishutumu Pakistan.
Uhusiano kati ya nchi hizo umedorora katika miaka ya hivi karibuni kutokana na shutuma kutoka Islamabad kwamba Afghanistan inahifadhi makundi ya wapiganaji.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.