Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Uharibifu wa kimbunga MelissaPicha: Ricardo Makyn/AFP
Jamaica imekumbwa na Kimbunga kikali zaidi cha Melissa kilichoambatana na upepo mkali na mvua kubwa na kuleta uharibifu katika taifa hilo la kisiwa kabla ya kuelekea Cuba.
Jamaica imekumbwa na Kimbunga kikali zaidi cha Melissa kilichoambatana na upepo mkali na mvua kubwa na kuleta uharibifu katika taifa hilo la kisiwa kabla ya kuelekea Cuba.
Waziri Mkuu wa Jamaica, Andrew Holness alitangaza kisiwa hicho kuwa eneo la maafa huku mamlaka zikitoa tahadhari kwa wakaazi kubaki mahali salama. Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameshuhudiwa huku hali ya hewa ikiendelea kuwa ya hatari.
Waziri wa serikali Desmond McKenzie alisema hospitali kadhaa zimeharibiwa, ikiwa ni pamoja na katika wilaya ya kusini-magharibi ya Saint Elizabeth, eneo la pwani ambalo alisema limefunikwa na maji.
Kimbunga hicho ni kibaya zaidi kuwahi kuikumba Jamaika, na kimepiga nchi kavu kwa upepo mkali wa kasi ya kilometa 300 kwa saa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.