Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Jeremy Knowles/Eventpress/picture alliance
Rais wa Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na viongozi wa nchi za Nordic wamesema wana imani ifikiapo Desemba kutafikiwa makubaliano ya kuvifadhili vita Ukraine kwa mali za Urusi zilizofungiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Von der Leyen aliyehudhuria mkutano wa viongozi wa Nordic huko Stockholm nchini Sweden, amesema kisheria wazo hilo la kuzitumia mali hizo ni wazo zuri. Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen amesema analiunga mkono kikamilifu wazo hilo.
Mpango huo lakini umepingwa pakubwa na Ubelgiji, ambayo ndiyo inayoshikilia sehemu kubwa ya mali zenye thamani ya yuro bilioni 200 za Urusi zilizofungiwa.
Ubelgiji inahofia athari za kisheria zinazoweza kutokea kutokana na hatua hiyo na usaidizi itakaopata katika kuubeba mzigo.
Pendekezo hilo litawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mwezi Desemba.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.