Uchumi huru,usiokuwa na majuto.

Utangulizi:

Makala haya ya UCHUMI HURU USIOKUWA NA MAJUTO, nimekutolea tena kwa lengo la yakusaidie katika mapambano ya kiuchumi, maana kama kuna eneo muhimu katika maisha ya mwanadamu ukitoa maisha ya kiroho lingine linachofuata ni uchumi, nimepata hadithi kuhusu Taifa la Marekani, jinsi linavyo jali na kuheshimu uchumi, Taifa la Marekani linamthamini sana mtu anayelipa kodi.

Na mtu yeyote asiyelipa kodi Marekani ina muhesabu kuwa kama adui mkubwa wa taifa hilo, ndani ya taifa hilo kama kuna sera zozote zinazopewa kipaumbele, sera ya kwanza inayopewa kipaumbele ni ya kulinda na kukuza uchumi wao.
Maana bila ya uchumi huwezi kufanya chochote kwa ufanisi mkubwa, tukisoma katika kitabu cha Muhubiri 10: 19 Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.

Ni kweli, maana pasipo fedha huwezi kuwa na ufanisi mzuri, pia huwezi kutawala pasipo fedha, huwezi kuendesha huduma au familia yako vizuri pasipo kuwa na fedha. Hivyo tunahitaji uchumi imara ili tuweze kuendesha maisha yetu kwa ujumla.

Mfano mzuri tukiangalia kwa upande wa huduma za kiroho, leo kuna watumishi wa Mungu wengi wazuri lakini hawajulikani, na sio kitu rahisi kuwajua kama ni watumishi wa maana, tatizo ni nini? Tatizo hawana pesa za kuzitangaza huduma zao.
Nataka kuthubutu kusema kwamba, hawa watumishi ambao unaowaona na kuwasikia katika maredio na luninga wengi wao sio wazuri kama wale wasiosikika, wengi wao wanaovuma sana hawana vipawa vya kuwashinda wale ambao hawavumi, wengi wanao vuma wanasaidiwa na nguvu ya fedha, tukisoma kitabu cha Mhubiri 9:13.16 Pia nimeona hekima chini ya jua, nayo ni kama hivi, tena kwangu mimi ilionekana kuwa ni neno kubwa.

Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.
Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.

Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.

Mtu yeyote anayechezea uchumi ni kama mtu anayechezea roho yake au uhai wake, uchumi ni kama roho au uhai, usiuchezee.
Kama unataka kuwa na maisha bora ni lazima kuheshimu swala zima la uchumi, hata kama unahitaji umtumikie Mungu vizuri ni lazima pia eneo la uchumi uwe umeonyesha kulijali
Maisha mazuri ya kiroho yanaenda sambamba na kuwa na uchumi bora.

Mungu alipotaka kuwatoa wana wa Israel katika utumwa nchini Misri, soma kutoka 3:8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

Malengo ya Mungu kuwatoa wana wa Israel utumwani Misri hayakuwa kwa ajili ya mambo ya kiroho peke yake, bali alikuwa na malengo ya kuwapa maisha bora, na mafanikio.
Mungu aliwaahidi kuwapa nchi njema yenye mafanikio tele yaani aliwaahidi kuwa na uchumi bora, rudia maneno haya, niwapandishe hata nchi njema tena pana nchi ijaayo maziwa na asali.

Maisha ya kiroho ili yafanikiwe ni lazima tumkabe ibilisi maeneo yote. Waefeso, 4:27 wala msimpe ibilisi nafasi. Kumbe ni lazima tumnyime nafasi ibilisi maeneo yote ya maisha yetu ya kiroho na kimwili. Mfano unaweza kuwa na maisha mazuri kiroho lakini katika eneo la uchumi hauko sawa, shetani anaweza kutumia nafasi hiyo hiyo ya kiuchumi kukujaribu na kuyaharibu maisha yako ya kiroho, rudia maneno haya Wala msimpe ibilisi nafasi.

Lakini hii haina maana au isidhaniwe kuwa nina maana iwapo mtu hajafanikiwa hawezi kumuabudu Mungu au hawezi kuookoka la! Mtu anapookoka ni sawa na wana wa Israel anasafiri kutoka Misri na kuelekea Kanani, kwa hivyo anaweza kuokoka akiwa maskini lakini anaelekea Katika Kanaani yake, yaani nchi ijaayo maziwa na asali ( kuelekea katika maisha ya mafanikio) Mimi kama mmoja wa Waumini na mwinjilisti wa makanisa ya Kiroho, maarufu kwa jina la Makanisa ya (Kipentekoste) tulikuwa na utaratibu kwa mtu yeyote akitaka kumtumikia Mungu, hasa katika huduma ya uchungaji. Ni lazima aache kazi zake zote, na hili lilikuwa ni kama sharti, kufanya kazi nje ya huduma huhesabika kama ni kosa kubwa.

Kupitia uelewa huo, inagharimu sana, pamoja na kutokujua kwa mtu
Mungu hawezi kuwaacha mwabuduo halisi kwasababu Mungu pia humsaidia mtu kwa rehema zake, ni kweli wengi huacha kazi zao,wakamua kuishi kwa kumtegemea Mungu na kutegemea sadaka za madhabahuni kuendesha maisha yao ya kila siku, na Kanisa wakati huo lilikuwa ni changa na lilikuwa na waumini wachache sana nao ni maskini.

Hata hivyo baada ya muda ,kuingiawakajipata katika,maisha ya shida yasio ya kawaida, lakini wakadhani ndio mapenzi ya Mungu wateseke hivyo kumbe sivyo.

Mchungaji mmoja alisema nami alivyokumbana na maisha ya shida.

Siku moja Mungu akaniambia nimfungulie mke wangu biashara, ili kwa hiyo biashara tujipatie walau riziki, ukweli nilishindana na sauti hii kwa muda mrefu, mwisho niliamua kumfungulia mke wangu biashara ndogo tu, lakini kwa yeye kwa kuwa alikuwa ni mama mchungaji haikunisumbua sana nikaona aah si mama mchungaji tu haina shida, baada ya kuwa na hiyo biashara baada ya muda mfupi tukaanza kuona maisha kuwa ahuweni tofauti na kwanza.

Baada ya miaka kadhaa Mungu akasema nami nilime bustani za mboga mboga, hii ndugu msomaji wangu haikuwa rahisi kwangu bali ilikuwa ni ngumu mno kuitii sauti hiyo, nilijiuliza mwenyewe maswali haya, yaani mimi mchungaji kabisaa watu wanione nalima pale? si watasema huyu sio mchungaji? Bali ni mchungaji njaa? Si watanidharau? Nk. Lakini Mungu akanisaidia akaniambia lima tu kuna mambo ninataka kukufundisha baadae.

Basi kwa wale walioko Kitale,eneo la Cherangany,kuwa na eneo kubwa la wazi ambalo lilifaa kwa kilimo nikamuona Daktari Mkuu wakati ule alikuwa Ipopo, baada ya kumuomba nilime kwa muda fulani eneo hilo kama kulisafisha, akaniruhusu, mara nilianza kulima bustani ya ajabu sana, ndani kulikuwa na kila kitu. Bilinganya, bamia, nyanya chungu, matango, pilipili hoho, na pilipili kali, mchicha, matembele, Spinachi (chaines) mnafu, kwa hiyo mtu akija pale anapata mboga zote nilikuwa naweza kuingiza siku moja sh. 10,000 na zaidi.

Maisha yakaanza kuwa mazuri kwakuwa mboga mboga ninazo, pia napata pesa kupitia mauzo ya mboga, huduma nayo ikazidi kwenda vema, watu walikuwa wananicheka lakini sikuathirika maana nilikuwa nakula nashiba, pesa nilipata na huduma ikawa inaendelea.
Mambo aliyonifundisha Mungu ni haya.

  1. Nisiwe na Utumishi wa kuiga bali niwe na Utumishi wa kusoma neno kwa Ufasaha, na kumsikiliza Mungu ili nijue kama anasema nini kuhusu huduma yangu?
  2. Mungu hawezi kumwambia mtu aache kazi bila ya kumtengenezea mazingira ya kupata mahitaji yake, hata wanafunzi wa Yesu walipoacha vyote kulikuwa na mazingira ambayo Yesu ameyaandaa ya kuwafanya wanafunzi kupata mahitaji yao.

Luka 22:35 Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!. Unaona hapo, ina maana wanafunzi walipotumwa ni kweli hawakuenda na mkoba wala chochote lakini kulikuwa na mazingira yaliyowafanya wapate mahitaji yao pasipo tatizo lolote

3 Mungu alinifundisha kwamba ijapokuwa kuna watu wengi wanafundisha kuhusu huduma kuu tano lakini bado hawaja fafanua jinsi hizo huduma zinavyo fanyakazi na wapi na kwa wakati gani?

Mfano ni kawaida kusikia Mchungaji anatumwa kwenda kufungua Kanisa jipya au kuanza kazi mahali ambapo hakuna mtu hata mmoja, yaani pasipo muumini hata mmoja ambaye tayari ameamini, kwa mujibu wa maandiko Mchungaji hawezi kufungua kanisa jipya, mtu anayepaswa kufungua kanisa jipya ni Mtume, Nabii, Mwinjilisti, lakini Mchungaji na Mwalimu hawapaswi kufungua Kanisa jipya, kwasababu Mchungaji hawezi kuwa Mchungaji bila ya kuwa na watu (Kondoo) na Mwalimu hawezi kufundisha miti, lazima kuwe na watu walioamini ili awafundishe.

Mwisho nikagundua kwamba mazingira niliyokuwa nafanyia kazi ya Mungu yalikuwa ni eneo la Mtume, kwa hiyo ni hivi, nilikuwa nafanya kazi ya Kichungaji mahali pa mtume.Omba Mungu akuonyeshe wito wako.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment