Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Octavio Jones/REUTERS
Umoja wa Mataifa unasema Jamaica itapigwa na Kimbunga Melissa, kimbunga kikali zaidi kuwahi kukipiga kisiwa hicho cha Caribbean katika karne hii.
Afisa mmoja wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa amesema kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha uharibifu mkubwa, mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Mamlaka nchini Jamaica zimetoa amri ya watu kuhama katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ukiwemo mji wa kihistoria wa Port Royal, na kuelekea maeneo salama kufuatia kimbunga hicho kitakachokuwa na upepo mkali wa kasi ya kilomita 300 kwa saa.
Kituo cha kinachohusika na Vimbunga cha Marekani, NHC, kinatarajia kimbunga hicho kiipige Jamaica leo kisha kipitie mashariki mwa Cuba halafu kitue Bahamas ifikiapo kesho Jumatano.
Waziri Mkuu wa Jamaica, Andrew Holness anasema serikali yake imejiandaa kwa hasara itakayotokana na kimbunga hicho ikiwa na bajeti ya dharura ya dola milioni 33.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.