Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Hazem Bader/AFP
Mamlaka za Israel zinasema zimewauwa wanamgambo watatu wa Kipalestina mapema leo wakati wa operesheni kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.
Katika taarifa, jeshi la Israel limesema wanamgambo hao walishiriki matukio ya kigaidi huko Jenin, mji ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi ila hawakutoa taarifa zaidi.
Haya yanafanyika wakati ambapo Israel imesema haitovikubaliavikosi vya jeshi vya Uturuki kuwa sehemu ya kikosi cha kimataifa kilichopendekezwa na Marekani, kusimamia makubaliano ya kusitisha vita vya Israel dhidi ya Hamas huko Gaza.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ziarani Hungary, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Israel, Gideon Saar amesema wanapinga kushiriki kwa Uturuki katika kikosi hicho kutokana na uhasama wa muda wa mrefu wa Rais Reccep Tayyip Erdogan dhidi ya Israel.
Saar vile vile amesema kuwa wameshaitaarifu Marekani kuhusiana na suala hilo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.