Wakenya wengi washawishiwa kupigana vita vya Ukraine

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Kremlin Press Office/TASS/ZUMA/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema hapo jana kwamba baadhi ya Wakenya wamekuwa wakishawishiwa ili kwenda kupigana upande wa Urusi katika vita vyake nchini Ukraine.

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema hapo jana kwamba baadhi ya Wakenya wamekuwa wakishawishiwa ili kwenda kupigana upande wa Urusi katika vita vyake nchini Ukraine. Katika taarifa iliyosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi, imebainisha kwamba Wakenya wengi wameishia kuzuiliwa katika kambi za kijeshi nchini Urusi.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba vitendo hivyo vinaendeshwa na mawakala na mafisadi ambao wanadai kufanya kazi na serikali na kuwalaghai Wakenya, wanaosafiri hadi Urusi na billa kujua wanajikuta katika operesheni za kijeshi za nchi hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haikutoa idadi yoyote ya Wakenya waliojiriwa, wangapi wamezuiliwa au kujeruhiwa. Mwezi uliopita, Wizara hiyo ya mambo ya nje, inadai kwamba ilifanya mkutano muhimu na maafisa wa Urusi ili kusaidia katika kuachiliwa na kurejeshwa kwa raia wake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment