Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais Paul Biya wa Cameroon akiwa na mkewe Chantal wakati wa upigaji kura katika mji mkuu Yaoundé: 12.10.2025Picha: Zohra Bensemra/REUTERS
Rais Paul Biya wa Cameroon ameshinda muhula wa nane madarakani katika uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 12 kwa kujipatia asilimia 53.66 ya kura.
Hii ikiwa ni kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa Jumatatu na Baraza la Katiba la Cameroon. Kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma Bakary ambaye ameambulia nafasi ya pili na asilimia 35,2 ya kura, amepinga matokeo hayo akisema hakukuwa na uchaguzi wa huru na haki.
Siku ya Jumapili, mamia ya raia wa Cameroon waliitikia wito wa kuandamana uliotolewa na Tchiroma, ambaye alipambana na Rais Paul Biya aliyeitawala Cameroon kwa miaka 43. Watu wanne wameripotiwa kuuawa kufuatia maandamano hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.