Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais Donald Trump alipowasili TokyoPicha: Philip Fong/AFP
Rais wa Marekani Donald Trump amekutana hii leo na waziri mkuu mpya wa Japan, Sanae Takaichi, mjini Tokyo kwa mazungumzo yanayohusu biashara na usalama.
Rais wa Marekani Donald Trump amekutana hii leo na waziri mkuu mpya wa Japan, Sanae Takaichi, mjini Tokyo kwa mazungumzo yanayohusu biashara na usalama.
Trump aliye ziarani barani Asia, amemweleza kiongozi huyo wa Japan kwamba Washington na Tokyo ni washirika wakubwa katika kiwango cha juu zaidi na wanatarajia kusaini mikataba kadha ya ushirikiano.
Takaichi amemkaribisha Trump katika makazi ya waziri mkuu mjini Tokyo, ikiwa ni mkutano wake wa kwanza wa ana kwa ana na kiongozi wa Marekani, siku chache tu tangu aingie madarakani.
Trump aliwasili Tokyo jana kwa ziara iliyoanzia Malaysia siku ya Jumapili. Rais Trump atakutana pia na Rais wa China Xi Jinping katika juhudi za kupunguza vita vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili kubwa kiuchumi duniani, vilivyochangiwa na ushuru mkubwa wa Marekani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.