Mali: Shule zafungwa kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mali imechukua hatua ya kufunga shule kutokana na uhaba mkubwa wa mafutaPicha: Idriss Sangare/REUTERS

Mamlaka za Mali zimechukua hatua ya kufunga shule na vyuo vikuu kwa muda wa wiki mbili kufuatia uhaba mkubwa wa mafuta.

Uhaba huo umesababishwa na vizuizi vilivyowekwa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda. Mapema mwezi Septemba, wanamgambo wa  Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM)  walitangaza kuzuia uagizaji wa mafuta katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi isiyo na bandari, na tangu wakati huo wamekuwa wakishambulia misafara ya malori ya mafuta yanayojaribu kuingia nchini humo.

Hatua hii inatajwa na wachambuzi kuwa ni sehemu ya kampeni ya makundi hayo ya wanamgambo na inayolenga kuzidisha shinikizo kwa serikali ya kijeshi ya  Mali kwa kuzuia chanzo kikuu cha uchumi nchini humo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment