Watu wawili wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Moshi ukifuka baada ya shambulizi la Israel huko Khan Younis kusini mwa GazaPicha: Stringer/REUTERS

Watu wawili wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa kusini mwa Gaza kufuatia shambulio la Israel katika mji wa Abasan al-Kabira.

Hayo yameelezwa na vyanzo kadhaa kutoka Hospitali ya Nasser huko Khan Younis. Jeshi la Israel limesema linafanya uchunguzi kuthibitisha au la taarifa hizo ambazo zinayaweka hatarini makubaliano dhaifu ya kusitisha  mapigano huko Gaza . Hii ni wakati Israel imesema Jumapili kuwa itaamua yenyewe ni wapi na lini itawashambulia maadui zake.

Hayo yakiarifiwa, familia za mateka wa  Israel  zimeitolea wito serikali yao, utawala wa Marekani na wapatanishi kusitisha awamu inayofuata ya makubaliano hayo ya amani hadi Hamas itakaporejesha miili ya mateka wote. Jukwaa hilo la jamaa wa mateka  limesema bado kuna miili 13 kati ya 48 ambayo haijareshwa na Hamas.

Tutumie maoni yako

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment