Norway: Urusi ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Aina ya makombora ya masafa marefuPicha: Shivansh Gupta/PA Wire/picture alliance

Idara ya ujasusi wa kijeshi ya Norway imesema Urusi ilifanya siku ya Jumapili jaribio la kombora la masafa marefu lenye uwezo wa nyuklia la Burevestnik.

Kombora hilo lilifyetuliwa kutoka visiwa vya Novaya Zemlya vilivyopo kwenye Bahari ya Aktiki. Moscow imesema jaribio hilo lilifanikiwa kikamilifu na kutaja kuwa kombora hilo lina uwezo wa kuepuka mifumo yote ya ulinzi. Hatua hiyo imekosolewa vikali na rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaka rais  Vladimir Putin  kumaliza vita vya Ukraine badala ya kujaribu makombora mapya.

Aidha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema anatarajia katika siku chache zijazo kwamba washirika wake wa Magharibi watawasilisha pendekezo la amani ili kukomesha vita vyake na Urusi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment