Mungu akiniambia sema na watu wangu watu waliofika mahali wakaona kwamba sasa nimefika mwisho
Sijajua ninani lakini Mungu amenisemesha ya kwamba wako watu ambao kibinadamu wamechoka na akili zao zimefika mwisho
Inawezekana ni kwenye mahusiano umeumizwa mpaka umefika mahali unasema nimefika mwisho sitaki tena,inawezekana ni kwenye ndoa akili zako zimefika mwisho
Moyo wako umejaa maumivu na uchungu uliopelekea hata chakula kukosa radha mdomoni mwako kwasababu ya akili kufika mwisho
Nikiwa katika kuomba na kusali nikasikia sauti ikiniambia sio mwisho, hata kama akili zimefika mwisho Mungu bado hajafika mwisho
Mahali akili za mwanadamu zinapoishia ndipo Mungu anapoanzia inuka tena, Mungu akupe nguvu mpya bado safari inaendalea hapo sio mwisho
Ninakuombea sana Mungu akupe nguvu ya kuinuka tena,ninekuombea Mungu akupe nguvu ya kuendelea tena kesho yako ni nzuri kuliko leo yako sio mwisho songa mbele.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.