Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Moja ya majaribio ya makombora ya masafa ya Urusi mnamo mwaka 2018Picha: RU-RTR Russian Television/AP Photo/picture alliance
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza Jumapili kuwa nchi yake inatarajia kufanya jaribio la kombora la masafa lenye uwezo wa nyuklia la Burevestnik.
Hatua hiyo ilikosolewa vikali na rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaka Putin kumaliza vita vya Ukraine : “Sidhani kama ni busara kwa Putin kusema hayo. Anapaswa kumaliza vita. Vita ambavyo vingechukua wiki moja sasa vinaelekea katika mwaka wake wa nne. Hilo ndilo analopaswa kufanya badala ya kujaribu makombora.”
Hayo yakiarifiwa, Urusi imesema imefanikiwa kudungua droni 193 zilizorushwa na Ukraine zikiwemo 34 zilizokuwa zimeulenga mji mkuu Moscow na 47 zikililenga jimbo la Bryansk ambako mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine watano wamejeruhiwa.
Hakukuripotiwa uharibifu mkubwa lakini shughuli zilivurugika huku viwanja vya ndege vikifungwa kwa muda katika vitongoji vya mji wa Moscow. Hata hivyo imekuwa nadra kwa Moscow kutoa taarifa kamili kuhusiana na mashambulizi ya Ukraine.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.