Marekani: Shambulio la Israel si ukiukaji wa mpango wa amani

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akizungumza na wanahabari nchini Israel: 24.10.2025Picha: Fadel Senna/UPI Photo/IMAGO

Marekani imesema Jumatatu kuwa shambulio la Jumamosi la Israel katika Ukanda wa Gaza si ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, baada ya Israel kutangaza kuwa ilifanya shambulio na kumlenga mpiganaji wa kundi la wanamgambo la Islamic Jihad ambaye alikuwa akipanga kushambulia vikosi vya Israel, madai yaliyokanushwa na kundi hilo.

Hayo yakiarifiwa,  Israel  imesisitiza Jumapili kwamba itaendelea kusimamia usalama ndani ya Gaza na kwamba itaamua yenyewe wapi na lini watawashambulia maadui zake. Chini ya masharti ya kusitisha mapigano, vikosi vya Israel vitatakiwa kuondoka Gaza huku kikosi cha kimataifa kinachotarajiwa kutoka nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu, kikitarajiwa kulinda usalama wa  Gaza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment