Watu wanne wauawa katika maandamano nchini Cameroon

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Wafuasi wa upinzani wakiandamana barabaraniPicha: Zohra Bensemra/REUTERS

Watu wanne wameuawa katika makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani wa Cameroon ambaye anadai kushinda uchaguzi wa hivi karibuni wa rais.

Mamia ya waandamanaji wa upinzani walifurika katika mikoa mbalimbali nchini Cameroon wakihimiza matokeo sahihi ya uchaguzi wa rais yanayotarajiwa kutangazwa rasmi Jumatatu na Mahakama Kuu.

Watu wanne wameuawa katika makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani anayedai kushinda  uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 12. Issa Tchiroma Bakary, ambaye alipambana na Rais Paul Biya aliyetawala kwa miaka 43, aliwataka wafuasi wake kuandamana kwa amani usiku wa kuamkia tangazo hilo, licha ya marufuku ya mikusanyiko ya umma.

Tchiroma anasema alishinda kwa asilimia 54.8 ya kura, lakini wachambuzi wengi wanatarajia kuwa Biya mwenye umri wa miaka 92 atajishindia muhula wa nane madarakani katika uchaguzi ambao wakasoaji wanasema umeshuhudia wizi wa kura.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment