ENDELEA KUFANYA HADI UPATE MATOKEO MAKUBWA.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Si kila mtu ataelewa unachokifanya sasa.

Wapo watakaoona unapoteza muda, wengine wakidhani unajifanya, na baadhi wakihisi hustahili kuifanya biashara hiyo au jambo hilo.

Lakini ukweli ni kwamba, unachohitaji ni ujasiri wa kusimamia kile unachoamini.

Hapo ndipo ulipo msingi wa mafanikio yako.

Siku moja, wale wanaokuona leo kama unapoteza muda, ndio watakaokuja kukuuliza ulifanikishaje.

Kwa hiyo endelea kusimama imara, fanya kazi kwa bidii, na usiogope kuonekana tofauti.

Mara nyingi, waliothubutu kuonekana tofauti ndio waliobadilisha maisha yao na ya wengine.

Kumbuka, safari ya mafanikio ni ya wale wanaothubutu, si ya wanaosubiri kueleweka.

Endelea kufanya, endelea kuamini, na matokeo yako yatakuwa ushahidi tosha.

Hadi sana ni …

Je, ni jambo gani bado linakusumbua kuanzisha biashara yako au kufanya ili kufikia mafanikio yako.?

Niandikie Kwenye comment hapa chini niweze kukusaidia.

Share ujumbe huu kwa watu wengine ili kupata uthubutu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment