Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Hali ya kibinadamu imezorota mji wa El Fasher SudanPicha: UNICEF/Xinhua/picture alliance
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa njia salama kwa raia waliokwama na wanaokimbia mji wa Sudan wa El Fasher, baada ya wanamgambo wa RSF kudai jumapili kuwa wanaudhibiti kikamilifu mji huo.
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa njia salama kwa raia waliokwama na wanaokimbia mji wa Sudan wa El Fasher, baada ya wanamgambo wa RSF kudai jumapili kuwa wanaudhibiti kikamilifu mji huo.
Mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher, alisema kuwa ameshutushwa na ripoti za vifo vya raia huko El-Fasher, ambako ilikuwa ni kituo kikuu cha mwisho cha magharibi mwa Darfur ambacho hakikuwa mikononi mwa RSF.
Fletcher amesema maelfu ya raia wanaendelea kunasa na kushikwa na hofu, kufa njaa kwasababu hawana chakula, huduma ya afya na usalama.
Aidha pia mkuu huyo ametaka mashambulizi dhidi ya raia, hospitali na operesheni za kiutu kukomeshwa mara moja. Kiasi cha watu 260,000, nusu yao wakiwa ni watoto wamekwama ndani ya El Fasher bila msaada wa chakula.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.