Trump aelekea Japan leo kabla ya mkutano wa kilele na Xi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Donald Trump akiwa na Mawaziri Wakuu wa Thailand na CambodiaPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/dpa/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump anaelekea Japan leo Jumatatu katika siku ya pili ya ziara yake barani Asia inayotarajiwa kukamilika kwa mkutano wa kilele na Rais wa China na Xi Jinping.

Rais wa Marekani Donald Trump anaelekea Japan leo Jumatatu katika siku ya pili ya ziara yake barani Asia inayotarajiwa kukamilika kwa mkutano wa kilele na Rais wa China na Xi Jinping.

Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Trump tangu arejee madarakani, ilianza jana jumapili nchini Malaysia kwa msururu wa makubaliano.

Makubaliano hayo yalijumuisha mikataba ya kibiashara kati ya majirani Cambodia na Thailand baada ya kusaini mkataba wao wa kusitisha mapigano kando ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-mashariki mwa Asia (ASEAN) huko Kuala Lumpur.

Trump pia alisaini mkataba wa biashara na madini na Malaysia, na kuamua kurekebisha uhusiano na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva baada ya miezi kadhaa ya mvutano.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment