Raia nchini Ivory Coast wapiga kura ya kumchagua rais mpya

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Kampeini za rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara mnamo Oktoba 18, 2025Picha: Joseph Zahui/Matrix Images/IMAGO

Raia nchini Ivory Coast leo Jumamosi wanapiga kura katika uchaguzi wa rais huku rais wa sasa Alassane Ouattara mwenye umri wa miaka 83, akiwania muhula wa nne, hatua itakayopanua utawala wake hadi karibu miongo miwili.

Wagombea wengine wanne pia wako kwenye kinyang’anyiro hicho cha urais nchini Ivory Coast.

Wapinzani wake wawili wakuu ambao ni rais wa zamani Laurent Gbagbo na Tidjane Thiam waliondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Ouattara atarajiwa kushinda katika raundi ya kwanza

Waangalizi wanatarajia Ouattara kushinda 50% ya kura zinazohitajika ili kujipatia ushindi katika raundi ya kwanza.

Taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo lina idadi ya watu karibu milioni 33, linakabiliwa na mvutano mkali wa kisiasa.

Upinzani na asasi za kiraia zinalalamika kuhusu vikwazo dhidi ya wakosoaji wa Ouattara na hali ya hofu.

Ukosefu wa ajira kwa vijana na rushwa ni masuala makubwa yalioangaziwa kwenye kampeni.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment