Kundi la Quad kufanya mkutano kuhusu Sudan mjini Washington

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Maafisa wa jeshi la Sudan waadhimisha miaka 71 tangu kuasisiwa kwa jeshi hiloPicha: AFP

Wawakilishi wa Marekani, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri wanakutana leo Ijumaa mjini Washington na pande husika katika vita vya Sudan, wakilenga kuzishinikiza kuelekea kwenye makubaliano ya amani.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mazungumzo hayo chini ya mwavuli wa Quad, mkutano huo utajadili njia za kuzitaka pande zinazopigana kuheshimu usitishaji vita wa miezi mitatu uliopendekezwa kote nchini Sudan.

Kundi hilo la Quad pia linafanya juhudi za pamoja kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika kwa waathiriwa wa mapigano.

Masuala yanayoshinikizwa na Quad 

Chanzo hicho kimeeleza kuwa wawakilishi wa mataifa hayo manne watakutana na pande hizo kwa nyakati tofauti.

Mwezi uliopita, Quad ilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuruhusu misaada kuingia Sudan humo, na kuweka msingi wa usitishaji wa kudumu wa vita pamoja na mpito kuelekea utawala wa kiraia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment