Ujerumani yaahidi kuisaidia Ukraine katika msimu wa baridi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Katherina ReichePicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Waziri wa uchumi wa Ujerumani Katherina Reiche amewasili nchini Ukraine leo pamoja na ujumbe wa kibiashara, na kuahidi msaada kwa Ukraine wakati wa msimu wa baridi unaokuja .

Baada ya kuwasili katika mji mkuu wa Kiev, Reiche amewaambia waandishi wa habari kwamba katikamsimu huo wa baridi, watafanya kila wawezalo kuhakikisha Ukraine inajikimu vyema.

Amesema watasaidia kujenga upya miundombinu ya nishati na kubadilisha vifaa vilivyoharibiwa pamoja na kikosi kazi chake kifedha na kiutaratibu, kwa ushirikiano wa karibu na wasambazaji wa nishati wa Ujerumani na Ukraine.

Urusi yashambulia kwa makusudi mifumo ya nishati ya Ukraine

Ameongeza kuwa tangu mwanzo, Urusi ililenga kwa makusudi mifumo ya usambazaji ya nishati ya Ukraine katika jaribio la kuwahujumu raia wake. Reiche amesema Ujerumani pia itatoa fedha za ziada kwa ajili ya ununuzi wa gesi asilia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment