Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Hadi sasa huna biashara ya kufanya? Angalia kulingana na eneo lako unaweza kufanya biashara gani kati ya hizi.?Chagua yako..
1.Biashara ya chakula
Chipsi, mishikaki, juice, kahawa, mama lishe n.k.Watu wengi wapo busy sana, hawana muda wa kupika. Kila mtu lazima ale, hivyo hii ni biashara ya uhakika.
..
2. Biashara ya vinywaji
Maji, soda, juisi, energy drinks n.k.
Watu hupata kiu muda wote, hasa joto likiwa kali. Mauzo ni ya haraka na mzunguko ni mkubwa.
..
3. Biashara ya nguo na fashion
Nguo za mitumba, nguo mpya kutoka China/Turkey.Sherehe ni nyingi sana na unaweza kuuza online au duka Kariakoo.
..
4. Biashara ya simu na vifaa vyake
Simu, charger, earphones, power banks, cover, screen protectors n.k.
Simu ni lazima kwa kila mtu, vifaa hivi vinauzika kila siku.
..
5. Biashara ya spear parts
Vifaa vya pikipiki, bajaji na magari.
Vyombo vya usafiri ni vingi sana kila sehemu hivyo sehemu ya spear parts ni fursa kubwa.
..
6. Biashara ya furniture ndogo
Meza, kabati ndogo, vitanda, sofa.
Watu wengi huanza maisha mahitaji ya vitu hivi yapo kila siku.
..
7. Biashara ya vitu used
Friji, TV, sofa, magari au vifaa vya ndani.
Bidhaa za used zinauzika sana kwa sababu ya bei nafuu.
..
8. Biashara ya vipodozi na urembo
Makeup, skincare, saloon za urembo.
Wanawake wengi, wanapenda mwonekano, ukitumia TikTok na Instagram utapata wateja wengi.
..
9.Huduma ya usafirishaji
Bodaboda, bajaji, delivery apps.
Biashara ya delivery imekua sana kutokana na online orders, ila inahitaji uaminifu.
10.Biashara ya udalali
Kuwasaidia watu kupata nyumba, viwanja, au magari.. Kila mji kuna fursa na watu wapya, udalali ni biashara ya mtandao mkubwa.
..
11. Biashara ya uwinga.
Watu wengi hutoka mikoani wakiulizia bidhaa. Ukiwaunganisha na maduka Kariakoo unapata faida kubwa.
…
12 Biashara ya Saloon
Saloon ya kike au kiume + vifaa vyake.
Kila mtu anapenda kuwa smart. Saloon ziko na wateja wa kudumu.
..
13.Biashara ya Vifaa vya Nyumbani
Vyombo, mapazia, mashuka, mito.
Watu kila siku wanapamba nyumba zao, hii ni biashara yenye mzunguko mzuri.
14. Biashara ya Online
Tumia TikTok, WhatsApp, Facebook, Instagram kutangaza bidhaa.
Hakuna gharama kubwa, ila mwendelezo na content nzuri ni muhimu.
..
15.Huduma za Stationery
Photocopy, printing, lamination, binding.
Shule na vyuo vipo vingi kila sehemu hii ni biashara yenye uhakika.
16. Biashara ya Viatu
Mitumba, viatu vipya, sports shoes, high heels, sandals.
Ni bidhaa ya lazima, mzunguko wake ni mkubwa.
…
17 Biashara ya Electronics & Solar
TV, radio, speakers, decoder, pamoja na solar equipment.Hii inalipa sana, hasa kwa kuwa watu wanakimbilia suluhisho la nishati mbadala.
..
18. Biashara ya Vifaa vya Ujenzi
Mabati, nondo, tiles, misumari, mabomba n.k. Kila sehemu sasa kuna ujenzi. Wateja ni wa jumla na rejareja.
..
19.Biashara ya Mafunzo na Ushauri (Coaching/Consulting)
Dar es Salaam kuna vijana na wafanyabiashara wengi wanaotafuta maarifa.Unaweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali, kompyuta, lugha, au huduma za ushauri (mfano kifedha, kisheria, masoko).
Hii ni biashara inayokua sana kwa sababu watu wako tayari kulipia taarifa zitakazowasaidia kufanikiwa.
…
20. Biashara ya Mafuta ya Kupikia & Nafaka
Uza mafuta ya kupikia, mchele, maharage, unga wa ngano na mahindi.
Hizi ni bidhaa za lazima, zinauzika kila siku bila kukosa wateja.
21. Biashara ya miamala ya simu.
Kila sehemu watu lazima watoe pesa na kutuma. Weka eneo lenye msongamano wa watu au kwenye soko au maingilio ya watu.
Biashara hii unaweza kuweka aina ya miamala ambayo ni pendwa sana kulingana na watu husika.
22. Biashara ya ufugaji .
Fuga kuku, ng’ombe na mifugo mingine utapata pesa .. mifugo inalipa kwa sasa ..
23. Biashara ya usafi ( Dry cleaners)
Watu wapo busy sana, weka ofisi ya kufua nguo na kufanya usafi majumbani.
24. Biashara ya mikopo ya fedha (micro finance)
Watu wengi wanataka mitaji ya kuanzisha biashara na kukuza biashara zao..wateja ni wengi mtaani.
25. Biashara ya ufundi.
Kuwa fundi bomba,nyumba,simu, fundi nguo n.k utapiga hela..ufundi kila siku ni dili.
Kabla haujaanzisha biashara yoyote Fanya utafiti, ili kuabaini ipi ni changamoto kwenye eneo lako na uweze kuitumia kama fursa.
Wewe unatamani kuanza na ipi?
Au ni biashara gani inafanya vizuri kwenye eneo lako ila haipo kwenye listi hii?
Andika hapa chini kwenye comment ili wengine pia wapate fursa…
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.