Stuttgart waangukia pua mikononi mwa Fenerbahce ya Uturuki

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mchezaji wa Stuttgart Jamie LewelingPicha: Ralf Brueck/Jan Huebner/IMAGO

Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, VfB Stuttgart imelazwa 1-0 na Fenerbahce ya Uturuki usiku wa kuamkia leo katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Ulaya.

Bao la fenerbahce lilifungwa na Kerem Aktürkoglu kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 34 ya mechi, baada ya Angelo Stiller kumuangusha Milan Skriniar. Hii ni mechi ya pili mfululizo Stuttgart kufungwa katika mashindano hayo.

Kocha wa stuttgart Sebastian Hoeness amesema wanatoka huko Uturuki wakiwa wanajivunia kwa mchezo mzuri walioucheza kwani ndivyo walivyopanga kucheza licha ya kuwa hakuweza kupata pointi tatu muhimu.

Fenerbahce ambao wanafunzwa na kocha raia wa Ujerumani Domenico Tedesco, kwa sasa wana jumla ya pointi sita baada ya kupata ushindi katika mechi yao iliyopita walipochuana na Dinamo Zagreb.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment