Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Makamu wa rais wa Marekani JD Vance na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff akiwa amesimama nyuma yakePicha: Francisco Seco/AP Photo/dpa/picture alliance
Makamu wa rais wa Marekani JD Vance, amelikosoa Bunge la Israel kwa kupitisha miswada ya kuuzingira Ukingo wa Magharibi.
JD Vance amesema hatua hiyo ni sawa na tusi na inaenda kinyume na sera za utawala wa Marekanina juhudi za kuhakikisha makubaliano ya amani kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas, yaliyosimamiwa na Rais Donald Trump, yanatekelezwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio aliyeshutumu hatua hiyo pia, amewaambia waandishi habari kwamba anapanga kuelekea Mashariki ya Kati na kuteua afisa wa kidiplomasia atakayeshirikiana na kamanda wa ngazi ya juu wa Marekani kwenye eneo hilo.
Kwingineko huko The Hague, Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, imesema ni sharti Israel iliruhusu Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina Gaza (UNRWA), kuendelea na shughuli zake za kiutu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.