Mabalozi wa EU wakubaliana kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Vikwazo hivyo vipya vinatarajiwa kuanza kutekelezwa kesho asubuhi.

Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wameridhia kuweka vikwazo vipya dhidi ya Moscow ili kukabiliana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Vikwazo hivi vinalenga kupunguza mapato ya mafuta na gesi ya Moscow, kulingana na Denmark, ambayo kwa sasa inashikilia urais wa EU.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kupiga marufuku uagizaji wa gesi asilia iliyoyeyuka kutoka Urusi hadi mwaka 2027, kuzipiga marufuku meli za mafuta zinazotumiwa na Moscow, na vikwazo vya kusafiri kwa wanadiplomasia wa Urusi kwenda Ulaya, AFP inabainisha.

Vikwazo hivyo vipya vinatarajiwa kuanza kutekelezwa kesho asubuhi.

Aidha, Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Washington pia hivi karibuni itatangaza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Urusi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment