Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Baraza la Katiba la Cameroon linasema kuwa litatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais siku ya Jumatatu tarehe 27 Oktoba, saa 11 asubuhi kwa saa za huko.
Haya yanajiri baada ya kuhitimisha kusikilizwa kwa kesi leo.
Majaji walitupilia mbali maombi yote ya ama kufutwa kwa sehemu au uchaguzi wote.
Hivi karibuni Kanisa Katoliki nchini Cameroon liliwataka majaji wa Baraza la Katiba kuhakikisha uamuzi wao unaonesha matakwa ya wapiga kura, likiomba kwamba matokeo yasibadilishwe ili kumpendelea mgombea mwingine.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, miji mikubwa nchini imekumbwa na maandamano, huku wengi wakikemea ukiukaji mkubwa wa zoezi la uchaguzi.
Msemaji wa zamani wa serikali Issa Tchiroma Bakary alijitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi huo na kumtaka Rais Paul Biya akubali kushindwa.
Mamlaka hiyo ilieleza hatua yake hiyo kuwa kinyume cha sheria na kuwataka wananchi kusubiri matokeo rasmi ya Baraza la Katiba.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.