Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Mashambulizi makali ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Urusi dhidi ya miji ya Ukraine yamesababisha vifo vya takriban watu sita, wakiwemo watoto wawili, Rais Volodymyr Zelensky amesema.
Watu wengine 21 walijeruhiwa, katika usiku mwingine wa mashambulizi ambayo alisema yalithibitisha kuwa Moscow haikuwa chini ya shinikizo la kutosha kwa kuendelea kwa vita.
Saa chache kabla ya hapo, Rais wa Marekani Donald Trump alistisha mpango wa kukutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa kilele unaotarajiwa kufanyika mjini Budapest, Hungary.
Trump alisema hataki “kupoteza muda”. Ikulu ya Kremlin imekataa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika uliyotolewa na Trump na viongozi wa Ulaya.
Huku hayo yakijiri jeshi la Ukraine limasema kuwa limeshambulia kiwanda cha kemikali cha Urusi katika eneo la mpakani la Bryansk usiku wa Jumanne kwa kutumia makombora ya Storm Shadow yaliyotolewa na Uingereza.
Shambulizi hilo “lililkuwa la kufana” kwa sababu lilipenya mfumo wa ulinzi wa anga wa Urusi, maafisa wa jeshi la Ukraine walisema.
Kiwanda cha Bryansk “kinazalisha baruti, vilipuzi na vifaa vinavyotumika kutengeza roketi na makombora yanayotumiwa na adui kushambulia eneo la Ukraine”.
Makumi ya watu wafariki katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria

Makumi ya watu wameripotiwa kufariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria baada ya gari hilo kuteleza kutoka barabarani na kuanguka, na kumwaga mafuta.
Wanakijiji walikimbilia eneo la ajali kuchota mafuta kutoka kwa lori lililopinduka lakini likapuka ghafla na kuwaka moto mkubwa uliowateketeza.
Takriban watu 30 waliripotiwa kufariki, huku wengine wasiopungua 40 wakipata majeraha ya moto viwango tofauti.
Moto huo mkali ulitewaketeza waathiriwa wengi kiasi cha kutotambulika, na waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya karibu kwa matibabu.
Ajali zinazohusisha magari ya mafuta hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, licha ya onyo kutolewa kuhusu ya hatari ya kuteka mafuta yaliyomwagika.
‘Waliofariki katika ajali Uganda ni 46’ – Polisi
Mamlaka za Uganda zinasema idadi ya waliofariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye Barabara Kuu ya Kampala–Gulu 46, kufuatia taarifa mpya kutoka kwa maafisa wa hospitali.
Maafisa wanasema baadhi ya waathiriwa waliodhaniwa kuwa wamekufa hapo awali walipatikana wakiwa wamezira na sasa wanapokea matibabu.
Wafanya kazi wa kutoa huduma za dharura wanashirikiana na maafisa wa afya kuthibitisha idadi hiyo na kutoa taarifa sahihi huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha mkasa huo.
Watu 63 wamefariki dunia baada ya mabasi kugongana kwenye barabara kuu ya Kampala-Gulu, Uganda

Takribani watu 63 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa kwa ajali iliyohususha magari manne katika Barabara ya Kampala na mji wa Gulu.
Ajali hiyo iliyotokea Jumatano asubuhi,katika Kijiji cha Kitaleba, ilihusisha mabasi mawili, Lori na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser, kwa mujibu wa ripoti ya awali ya polisi.
Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka kutokana na baadhi ya abiria kujeruhiwa vibaya.
“Inaelezwa kuwa basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa likilipita lori na basi jingine lililokuwa likielekea Kampala lilikuwa likiipita gari ndogo ya Toyota Land Cruiser, lakini lilishindwa kufanya hivyo kwani tayari basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa limekaribia’’. Taarifa ya polisi imeeleza.
Hali ya wasiwasi yaongezeka nchini Cameroon, serikali yawakamata waandamanaji kadhaa

Serikali ya Cameroon inasema waandamanaji kadhaa wametiwa mbaroni katika mji wa kaskazini wa Garoua, ngome ya mgombea wa upinzani Issa Tchiroma Bakary, huku kukiwa na hofu kuhusu uwezekano wa ghasia nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa leo, Waziri wa Mambo ya Ndani Paul Atanga Nji alisema “wasumbufu” waliokamatwa walitumiwa na wachochezi kutoka ndani na nje ya nchi. “Kati ya watu waliokamatwa, 20 watapelekwa katika mahakama za kijeshi kujibu kwa vitendo vya uasi na uchochezi wa uasi,” Nji alifichua, akiongeza kuwa wengine walipelekwa katika mji mkuu wa Yaoundé kwa uchunguzi zaidi.
Hatua hiyo inafuatia mfululizo wa maandamano huko Garoua na Yaoundé leo, ambapo washiriki walishutumu hitilafu za uchaguzi na kueleza kumuunga mkono Tchiroma ambaye alidai ushindi katika uchaguzi wa rais.
Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha makundi yakiandamana na mabango yenye picha ya msemaji wa zamani wa serikali ambaye sasa anataka kumvua madaraka mkuu wake wa zamani Paul Biya.
Maafisa wa utawala katika tarafa ya Benoue ambako Garoua iko, wamepiga marufuku mzunguko wa pikipiki za kibiashara kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja asubuhi kwa saa za ndani.
Ilifuatia maandamano ya Jumatatu usiku na mamia ya waendesha baiskeli ambao waliingia barabarani katika kuonesha uungaji mkono kwa Tchiroma, kiongozi wa chama cha Cameroon National Salvation Front.
Katika siku za hivi karibuni, maafisa wa utawala, watawala wa kimila, mashirika ya kidini na ya kiraia wameomba utulivu wakati nchi ikisubiri matokeo ya uchaguzi wa urais.
Huku wengi wakiazimia kutetea kile wanachodai ukweli wa kura, kuna wasiwasi kwamba huenda taifa likakumbwa na misukosuko ya baada ya uchaguzi.
Israel yapokea miili miwili ambayo Hamas inasema ni mateka waliokufa

Israel imepokea miili miwili ambayo Hamas inasema ni mateka wengine wawili waliofariki ambao walikuwa wamezuiliwa huko Gaza.
Jeshi la Israel limesema majeneza mawili yalikabidhiwa kwa wanajeshi katika ardhi ya Palestina na shirika la Msalaba Mwekundu ambalo hapo awali lilipokea kutoka kwa Hamas.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema majeneza hayo, ambayo yalisindikizwa na wanajeshi, yalikuwa yamevuka hadi Israel na yatachukuliwa kutambuliwa rasmi Tel Aviv.
Kuthibitishwa kwa utambulisho wao kutamaanisha kuwa Hamas imewahamisha mateka 15 kati ya 28 wa Israel waliofariki dunia chini ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani mapema mwezi huu.
Mateka wote 20 walio hai waliachiliwa muda mfupi baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.