Waasi wa M23 wapora dhahabu zenye thamani ya dola milioni 70

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mgodi wa dhahabu huko Kivu Kusini mashariki mwa DRCPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Kampuni moja ya uchimbaji madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema waasi wa M23 wamepora takriban kilo 500 za dhahabu ambazo thamani yake inakadiriwa kufikia dola milioni 70.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa uporaji huo umefanyika kuanzia mwezi Mei mwaka huu wakati M23 ilipochukua  udhibiti wa mgodi wa Twangiza uliopo Kivu Kusini na kwamba baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Twangiza Mining walihusika katika vitendo hivyo.

Kundi hilo la waasi wa M23 linaloungwa mkono na Rwanda halijazungumzia chochote juu ya taarifa hiyo, lakini kampuni ya Twangiza Mining imesema inajiandaa kuwasilisha malalamiko rasmi kwa mamlaka za Kongo na kwa makundi ya wapatanishi wa kimataifa, ikiwashutumu  waasi hao wa M23  kwa kuwafukuza wakaazi, kubomoa makanisa na kutumia wataalam wa Rwanda kutanua eneo la uchimbaji.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment