Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Marais Trump na Putin walitakiwa kukutana Budapest lakini mkutano huo umesitishwaPicha: ZED
Mkutano uliokuwa ukitarajiwa kufanyika kati ya marais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin huko Budapest Hungary, umesitishwa kwa muda baada ya Urusi kutupilia mbali suala la kusitisha mapigano.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio baada ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov. Trump amethibitisha taarifa hiyo akisema haitaji kuwa na mkutano usio na tija wala kupoteza muda.
Urusi kwa upande wake imesema maandalizi ya mkutano huo kati ya Trump na Putin yanaendelea lakini kwanza kunahitajika kukubaliana katika mambo kadhaa muhimu. Ikulu ya Kremlin imetoa tangazo baadaye na kusisitiza kuwa masharti yake ili kufikia amani nchini Ukraine bado hayajabadilika.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.