Kazi ya haki ya Umoja wa Mataifa yakabiliwa na kitisho

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Kamishena wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TürkPicha: Yamam Al Shaar/REUTERS

Shughuli za utetezi wa haki za Umoja wa Mataifa zinalengwa kupunguzwa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kifedha.

Hatua hii inatishia uchunguzi muhimu na juhudi za uwajibikaji. Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Huduma ya haki za kibinadamu, ISHR.

Shirika hilo linasema hatua ya Marekani kutolipa ada yake ya uanachama ya Umoja wa Mataifa pamoja na juhudi za China na Urusi kuondoa ufadhili wa mashirika ya kuetetea haki, ni mambo yanayoweza kuwa pigo kwa mapambano ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya ukiukaji wa haki.

Shirika hilo pia limesema kuwa tayari uchunguzi wa ngazi ya juu ulioamrishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kuhusiana na machafuko yanayoikumba Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, umeshindwa kufanyika kutokana na ukosefu wa fedha.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment