Uwanja wa ndege Khartoum washambuliwa kwa droni

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Ndege zilizoharibiwa na mashambulizi ya jeshi katika uwanja wa ndege wa KhartoumPicha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Khartoum umeshambuliwa kwa droni mapema leo, siku moja kabla serikali inayoungwa mkono na jeshi nchini humo kuufungua rasmi uwanja huo kwa ajili ya safari za ndani ya nchi.

Kuanza kwa safari hizo itakuwa mara ya kwanza tangu zaidi ya miaka miwili.

Mashuhuda wameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa wamesikia sauti za droni katika maeneo ya kati na kusini mwa Kahrtoum pamoja na milipuko katika eneo la uwanja wa ndege kuanzia saa kumi asubuhi hadi saa kumi na mbili.

Uwanja huo wa ndege umefungwa tangu mapigano yalipozuka Aprili 2023 kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF na kusababisha miundombinu muhimu kuharibiwa katika mji huo mkuu.

Khartoum imekuwa na utulivu tangu jeshi lilipochukua udhibiti mapema mwaka huu, ila mashambulizi ya droni yameendelea, huku wanamgambo wa RSF wakituhumiwa kuilenga miundombinu ya kijeshi na kiraia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment